ROYAL TOUR YA RAIS SAMIA YAZAA MATUNDA YA TAWTO.

 

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mohamed Mchengerwa na Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi wameungana na wadau wa sekta ya utalii jijini Arusha leo usiku huu April 14, 2023, kuzindua Chama cha Waongoza Utalii Wanawake (TAWTO) kinacholenga kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Wizara kutangaza Utalii kama Mhe Rais alivyofanya katika filamu ya Royal Tour.

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Ndug. Anderson Mutatembwa.

“ Sekta ya utalii mtarajie ushirikiano mkubwa kutoka kwangu na timu yangu kuliko wakati wowote katika kuhifadhi na kutangaza utalii,” alisema Mhe. Mchengerwa.

Ametoa rai kuwa madhumuni ya Chama hicho ni muhimu yaende sambamba na kuhamasishana kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za kuendesha shughuli za utalii nchini hususan Sheria ya Utalii ya Mwaka 2008 na kanuni zake. Pamoja na kuzingatia muongozo wa maadili kutoka Shirika la Utalii Duniani (UNWTO).

Aidha amesisitiza kuwa wabunifu zaidi katika kuandaa vifurushi vya safari za watalii (Tour Packages) ambavyo zitafungamanisha vivutio na mazao mbalimbali ya utalii kama fukwe, michezo, mikutano na matukio, Utamaduni na Utalii wa vyakula ili kuvutia watalii wengi zaidi, kuongeza idadi ya siku za wageni kukaa nchini na hivyo kuongeza mchango wa utalii katika Pato la Taifa.

Pia, ametilia mkazo utoaji wa huduma bora katika sekta yetu ya utalii na ukarimu ambapo amesema hatua hiyo itasaidia nchi yetu kuongeza idadi ya watalii na watalii kurudi kutembelea Tanzania.

Hapa naomba nisisitize makundi yanayohudumia watalii kama Waongoza Watalii (Tour Guides) na wafanyakazi katika tasnia ya ukarimu na huduma za malazi. Hawa ndio wanaokaa na wageni muda mrefu zaidi na hivyo ndio hasa mabalozi wa utalii wetu. Ni vema kuweka utaratibu mzuri wa kujenga uwezo kwa makundi haya ili kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo na kwa weledi. hali kadhalika, kwa kuzangitia kuwa sekta ya utalii kwa kiasi kikubwa inaendeshwa na sekta binafsi Serikali iliona umhuhimu wa wadau wa utalii kuwa na shirikisho la vya waendeshaji utalii yaani TCT, kwa msingi huo nitoe wito kwa chama chenu kujiunga na kushirikiana kikamilifu na shirikisho hilo (TCT), kwa mukthaza mzima wa kundeleza na kukuza sekta ya utalii nchini" amesisitiza, Mhe. Mchengerwa

Awali Mhe. Mchengerwa ameeleza kwamba Sekta ya utalii ni moja ya Sekta zilizoathirika zaidi na janga la UVIKO-19. Hata hivyo, kutokana na juhudi za Serikali ya awamu ya sita na wadau wa Sekta binafsi hali ya sekta imeanza kurejea katika hali yake, ambapo pia amesema idadi ya Simba imepanda na kukadiliwa Tanzania kuwa na zaidi ya Simba 17000 kwa sasa.

"Mathalan, kwa mwaka 2022, idadi ya watalii wa nje imeongezeka hadi kufikia 1,454,920 na mapato yatokanayo na utalii kufikia Dola za Marekani Milioni 2,527,77. Idadi ya watalii wa ndani wanaotembelea maeneo ya hifadhi imefikia 2,363,260. Ni wazi kuwa bado tuna kazi kubwa ya kuendelea kushirikiana katika kukuza utalii wa ndani lakini pia kutengeneza vifurushi vya utalii vya gharama nafuu ili kuhamasisha utalii wa ndani. Lengo la Serikali ni kufikia watalii milioni 5 na mapato yatokanayo na utalii kufikia bilioni 6 ifikapo mwaka 2025." Amehitimisha Mhe. Mchengerwa
Na John Mapepele

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments