RPC PWANI AHIMIZA MATENDO MEMA KWA JAMII

Kutoka Kulia mwenye sutu  ni RPC wa Mkoa wa Pwani Pius Lutumo  anayefuata ni Sheikh wa Mkoa wa Pwani  Alhaji  Abbas Mtupa  akimkabidhi zawadi mtoto mmoja kweye hafla hiyo ya Iftar
Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
KAMANDA wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani ACP Pius Lutumo jioni Aprili 18 amendaa Iftar kwa ajili ya watoto yatima na wenye mahitaji maalumu iliyofanyika kwenye Ukumbi Bwalo la Maaskari maarufu kama Maisha Plus Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

RPC Lutumo amesema anamshkuru Mwenyezi Mungu kwa kuwakutanisha mahali hapo wakiwa na afya ikiwa ni muendelezo wa Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuyakumbuka makundi haya maalumu na kuandaa Iftar kwa ajili yao kama jinsi tulivyoona wiki moja iliyopita ambapo Iftar maalumu iliandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge ambaye alisema wazi kuwa Iftar ile imetolewa na Mheshimiwa Rais Samia.

"Hivyo basi sisi Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani tumeona tumuunge mkono Rais wetu katika hili huku tukiwa na baraka zote kutoka kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IJP) Kamanda Camilius Wambura ambaye muda mchache uliopita nimeongea nae kwa njia ya simu na kumweleza kuwa sisi tupo kwenye Iftar ambayo tumeiandaa na taarifa anazo amefurahi sana na anawasilimia wote na kuwatakia Ramadhan Karim na maandalizi mema ya sikukukuu ya Eid El Fitr huku amewaasa wakaazi wa Mkoa wa Pwani kusherehekea kwa amani ikiwemo kuzingatia utii bila shuruti kwa kuto vunja amani.

RPC Lutumo amewashukuru Kamati ya Maandalizi walioratibu Iftar hiyo pamoja na wadau mbalimbali waliowawezesha kwa kutoa sadaka hiyo huku Jeshi la Polisi wakiwa ni daraja.

"Hii ibada ya kutukutanisha sisi pamoja tukumbuke kuwa sisi wote ni wa Mwenyeezi Mungu na kwake tutarejea hivyo tuishi maisha ya kumpendeza Mungu.

"Kwa kupitia mawaidha ya viongozi wetu wa dini na katika imani zote kwa kukataza matendo maovu kwani katika dini hukatazamambo mengi ambayo ni dhambi huku kwa upande wetu sisi Askari huita vitendo vya uhalifu, kimsingi Jeshi la Polisi tunafanya kazi ya aina moja yenye kusimamia mate ndo ya kumpendeza Mungu amesema Kamanda Lutumo.

" Nitoe wito kwa jamii kuwapends watoto na vijana yatima na wenye mahitaji maalumu jana Askari wa Wilayani Kibaha wametoa msaada kwenye vituo viwili vyakulelea watoto yatima na wenye mahitaji maalumu baadhi ya vitu walivyovitoa ni pamoja na Mbuzi mmoja ,Michele Kg.100,

Maharage Kg.50, Tende Boksi kubwa 2, Sukari Kg.40, Chumvi katuni 5, Sabuni ya kufulia,  kiroba kimoja, Sabuni za Vipande Boxi tatu, Mafuta ya kula lita 30, Unga wa Sembe Kg.75, Juisi parti 5, Pipi pakti5 na fedha taslimu kiasi cha 120,000.

Naye Sheikh wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abbas Mtupa ametoa pongezi kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa kuwa na muendelezo wa kuwakumbuka watoto yatima takriban miaka mitano sasa wamekua wakifanya hivyo huku akilishukuru Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwani kwa kufanya hivyo wanajemga uhusiano mzuri baina yao na jamii kwa ujumla.

"Wengi tunasahau umuhimu wa makundi haya ya watoto yatima kwani hawa ni kundi lenye thamani sana hapa duniani kwa sababu hawa nifunguo za peponi endapo tutawatendea mema pia ni funguo za motoni kwa wale wote wanao kula na kudhulumu mali ya yatima" amesema Sheikh Mtupa.

"Tulisaidie hili kundi na kila mtu akitaka kupata baraka ndani ya nyumba yake basi na amchukue yatima amlee kwa moyo wa upendo wa dhati atapata baraka na kuondolewa mabalaa na mikosi katika maisha yake ya kila siku" amesema Sheikh Mtupa.


RPC wa Mkoa wa  Pwani  Lutumo  akizungumza kwenye hafla hiyo ya Iftar

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments