Sababu ya Naibu Spika Zungu kumsamehe Bulaya

Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya ameingia kwenye mvutano na Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu baada ya kukaidi agizo lake.

Zungu amesema kitendo cha kupiga kelele na kutonyamaza hata alipotakiwa, ni ukiukwaji wa kanuni za Bunge na angeamua kutumia kanuni ya 84, ingemtoa nje mbunge huyo hata miaka mitatu.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Aprili 19, 2023 wakati akiahirisha kikao cha Bunge mchana kufuatia mvutano uliokuwa umejitokeza kabla.


Wawili hao walianza mvutano wakati Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Matiko alipokuwa akichangia kwenye Hotuba ya Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Utumishi na Utawala Bora Kwa mwaka 2023/24.

Wakati Matiko akiendelea na mchango wake, wabunge wengi kutoka CCM walisimama na kumpa taarifa kitendo kilichotafsiriwa na Bulaya kama kumpotezea muda mwenzake.

"Mheshimiwa Bulaya, naomba unyamaze, Bulaya nataka unyamaze na nikitumia mamlaka yangu naweza kukuondoa hapa ukajikuta umekaa nje hata miaka mitatu," amesema Zungu.

Wakati akihitimisha, Naibu Spika huyo amesema wabunge hao ni marafiki na yeye (Zungu) lakini akiwa mbele ya Siwa ni mtu mwingine na anaweza kutumia nguvu hiyo.

Amesema alishaamua kuchukua uamuzi huo lakini kutokana na kipindi hiki yuko kwenye mfungo ameamua kumsamehe mbunge huyo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments