Serikali kutoa vibali vya ajira 43,464

Serikali imesema itatoa vibali vya ajira ili kujaza nafasi 43,464 zilizoidhinishwa  kwenye mwaka 2023/2024.

Katika mwaka 2022/2023, Serikali ilitoa vibali vya ajira mpya 30,000 na vibali vya ajira mbadala 7,721 kwa waajiri kutoka katika taasisi mbalimbali vimetolewa.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Aprili 19, 2023 na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene.


“Itashughulikia vibali vya ajira ili kujaza nafasi 43,464 zilizoidhinishwa katika Ikama,”amesema.

Amesema pia watahakiki na kuidhinisha madai ya malimbikizo ya mishahara na kusahihisha taarifa zinazohusiana na masuala ya kiutumishi na mishahara ya watumishi kwa taasisi 433.

Aidha watakagua orodha ya malipo ya mshahara katika taasisi 150.

Katika mwaka 2023/2024, ofisi hiyo imeliomba Bunge kuwaidhinishia Sh1 trilioni kwa ajili ya mafungu yake sita ya bajeti.

Mafungu hayo ni Ofisi ya Rais Ikulu, Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, na Sekretarieti ya katika Utumishi wa Umma.

Mafungu mengine ni Tume ya Utumishi wa Umma na idara ndogo ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments