Sheikh Yunusi amesema hayo leo Aprili 22 katika hotuba ya ibada ya Iddi El Fitr iliyoswaliwa katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
“Tuyahifadhi madarasa tuliyopata katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Tulikuwa tunamuogopa Mungu basi tuendelee kumuogopa na tuendelee kutoa sadaka katika kila la kheri tusirudi nyuma, lakini haimaanishi tusipange mipango bali isiwe mipango mibaya na yenye kulipiza kisasi,” amesema Sheikh Yunusi.
Akizungumza baada ya ibada hiyo Mbunge wa Kondoa mjini Ally Makoa aliwataka viongozi wa dini kusimamia na kutoa elimu kuhusu mmomonyoko wa maadili nchini.
Makoa alisema huu si wakati wa vijana kukaa vijiweni bali wajitume kufanya kazi kwa bidii ili kuepuka mmomonyoko wa maadili ambayo sababu inawezekana ni kukosa kazi ya kufanya huku aiwasisitizia viongozi wa dini kuendelea kutoa elimu kuhusu mmomonyoko wa maadili.
Kwa upande mwingine, Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu ameitaka jamii kujitafakari ni kwa nini matendo ya ukatili wa kijinsia yanaongeza ndani ya jamii ikiwa watu wanaofanya matendo hayo wanaishi nao.
Akizungumza leo katika ibada ya Eid el Fitri katika msikiti wa Gaddafi jana jijini hapa, Sheikh Rajabu amesema watoto wanatakiwa kulelewa na kupewa elimu ya dini ili waweze kujua madhara ya ukatili wa kijinsia, lakini jambo la ajabu wanaofanya hayo wanatoka kwenye familia hizo.
"Ukatili unapatikana ndani ya familia zetu hili ni lazima tuliangalie kwa undani tatizo ni nini,kipi kifanyike,tushirikiane kwa pamoja hili ni la kwetu kwani linasababishwa na ukosefu wa maadili," amesema sheikh huyo.
Amesema waliofunga mwezi mtukufu wa Ramadhan wana wajibu wa kuendelea kutenda matendo mema ili kuendelea kupata nusra za Mwenyezi Mungu lakini kuwa kielelezo hata cha vita ya ukatili ambayo imeanza kutajw akila kona nchi.
0 Comments