Simba ‘Bob Junior’ aombewa filamu

Mbunge wa Hai Saashisha Mafue (CCM) ameihoji Serikali ni lini itaandika au kutengeneza filamu kuhusu ukoo wa Simba Bob Junior.

Mafue amesema historia hiyo inaweza kuwa kivutio kikubwa kutoka kwa wageni na watalii wanaotembelea nchini Tanzania ili waweze kujua historia yake.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Michezo na Utamaduni Hamisi Mwinjuma amesema jambo hilo linahitaji ushirikishwaji wa pamoja kati ya wizara mbili.


Kwa mujibu Mwinjuma, Wizara zinazotakiwa kukutana pamoja na kujadiliana kwenye matengenezo ya filamu au kitabu hicho ni Wizara ya Habari na Utamaduni na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Samba junior aliuawa mapema mwaka huu na waliodaiwa ni watoto wake katika Mbuga ya Serengeti kwa kilichodaiwa ni ugomvi wa kugombania ufalme.

Ni simba ambaye alikuwa kivutio kikubwa kwa wageni wanaotembelea hifadhi hiyo na alipata umaarufu mkubwa kutokana na muonekano wake.

Post a Comment

0 Comments