SIMBA SC YAIKANDA YANGA SC 2-0, YANGA BADO YUPO KILELENI

 




KLABU ya Simba imeweza kufuta uteja mbele ya mahasimu wao Yanga Sc mara baada ya kufanikiwa kuichapa 2-0 kwenye mchezo ambao umepigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Simba Sc ilianza kupata bao la mapema kabisa kupitia kwa Henock Inonga kabla ya Kibu Denis kumaliza mchezo kwa kupachika bao kali na kufanya matokeo kuwa 2-0.

Yanga Sc sasa itaendelea kuwa kileleni mwa ligi ikiwa na pointi 68 wakiwaacha mahasimu wao kwa pointi tano ambao kwa ushindi wa leo unawapeleka kuwa pointi 63.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments