KLABU ya Simba imefanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Wydad Cassablanca katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika
Mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam tumeshuhudia kandanda safi kutoka kwa wenyeji Simba sc ambao walitawala mchezo na kufanikiwa kupata bao la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wao raia wa DR Congo Jean Baleke akipokea pasi kutoka kwa Kibu Dennis kipindi cha kwanza.
Mpaka mapumziko Simba Sc ilikuwa mbele kwa bao moja ambalo walililinda mpaka dakika 90 na mpira kumalizika waki mbele kwa 1-0 hivyo kusubiri mechi ya marudiano ambayo itapigwa kwenye mji wa Wydad juma lijalo nchini Morocco.
Simba Sc ilianza na wacheza ambao walianza katika mechi ya wikiendi iliyopita dhidi ya watani wao wa jadi Yanga na kufanikiwa kupata ushindi.
0 Comments