SIMBA YADONDOKEA PUA UARABUNI, YANYUKWA KWA MIKWAJU YA PENATI 4-3

KLABU ya Simba imetolewa na Wydad Casablanca kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAF CL). baada ya kupokea kichapo kwa mikwaju ya penati 4-3 mara baada ya matokeo kuwa 1-0 (agg 1-1)


Katika mchezo huo ambao Simba alikuwa na faida ya bao moja mbele, waliingia uwanjani na kikosi kilekile kilichoanza mkondo wa kwanza Jijini Dar es Salaam ambacho kiliwasaidia kuondoka na ushindi wa bao 1-0.

Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Mohamed V nchini Morocco Wyadad waliweza kumuanzisha mshambuliaji wao hatari raia wa Senegal Bouly Sambou ambaye alionesha uhatari wake na kuweza kupata bao dakika ya 24 ya mchezo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments