Tarimba adai anayewania jimbo lake anakwamisha hospitali

Mbunge wa Kinondoni Tarimba Abbas (CCM) amedai kuwa kuna kigogo anazuia ujenzi wa hospitali katika jimbo hilo kwa nia ya kutafuta ubunge 2025.

Hata hivyo, Tarimba amesema huyo anayetaka kufanya hivyo anamkaribisha kupambana naye lakini asitumie njia ya kuzua ujenzi wa hospitali ambayo ni huduma kwa wananchi.

Tarimba ametoa kauli hiyo leo Jumanne April 18, 2023 wakati akichangia kwenye hotuba ya Makadilio ya Mapato na matumizi kwa Wizara ya Tamisemi kwa mwaka 2023/24 ambapo ameomba apelike jina kwa Waziri.


“Tunataka kujenga hospitali katika jimbo letu, lakini kuna mtumishi wa ngazi ya juu anazuia hospitali hiyo isijengwe, kwa sababu anataka kujijenga kisiasa katika safari ya kuusaka ubunge kwenye uchaguzi 2025, nasema aje tu namkaribisha tukutane,” amesema Tarimba.

Hata hivyo, hakumtaja kigogo huo wala eneo analofanyia kazi licha ya kukiri kuwa anamfahamu vizuri na amejiandaa kukabiliana naye wakati utakapofika.

Kwa mfumo wa CCM, kwa sasa wagombea hawaruhusu kujipitisha kwa wapiga kura na watakaobainika huwa wanajiweka katika hatihati ya kukatwa majina yao wakati utakapofika.

Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani utafanyika nchini kote mwaka 2025 ambapo vyama vya siasa vitakuwa na nafasi ya kuwanadi wagombea wao baada ya michakato ya uchaguzi wa ndani.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments