UVCCM kuingia shambani kuwatia moyo vijana mradi wa BBT

Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) unatarajia kuanzisha utaratibu wa kukutana na kuzungumza na vijana mara kwa mara kuhusu changamoto zinazowakabili.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Saaam, Ijumaa Aprili 14, 2023 na Katibu Hamasa na Chipukizi wa UVCCM Taifa, Edna Lameck baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi tangu alipoteuliwa na Baraza Kuu la jumuiya hiyo.

"Mwenyekiti ataweka utaratibu mzuri kuhakikisha anakutana mara kwa mara na vijana mbalimbali kubadilishana mawazo na uzoefu kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili," amesema.


Mbali na hilo, amesema Aprili 17, mwaka huu jumuiya hiyo inatarajia kuanza ziara katika Mikoa sita, kutembelea mradi wa Jenga Kesho iliyo Bora (BBT).


"Mwenyekiti atafanya ziara hii akiambatana nami kihakikisha umma inaelezwa na kuonyesha kile kinachofanywa na vijana wenzao ili nao wahamasike," amesema.


Edna aliteuliwa na Baraza Kuu kushika wadhifa huo, Machi 2023 akichukua nafasi ya Burugu Majenge aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo.


Mbali na Edna makabidhiano ya ofisi pia yamefanyika kwa nafasi ya Katibu wa Oganaizesheni, Mbarouk Mbarouk, aliyechukua wadhifa kutoka kwa Anzuruni Mtengwa.

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments