UVCCM yataka halmashauri kutenga maeneo ya kilimo kwa ajili ya vijana

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Mohammed Kawaida amezitaka halmashauri zote nchini, kuandaa maeneo maalum ya mashamba kwa ajili ya vijana.

Kawaida ameyasema hayo leo Jumanne, Aprili 25, 2023 katika ziara yake ya kutembelea mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT), katika Chuo cha Mafunzo ya Kilimo Kilimanjaro.

Hatua hiyo, amesema inalenga kuandaa maeneo yatakayotumika na vijana kwa ajili ya kilimo kwa kuwa ndiyo msingi wa uchumi wa nchi.


"Hii inatokana na ukweli kwamba wazo la Rais Samia Suluhu Hassan la kuilisha dunia halitatimia kama hatutakuwa na ardhi ya Kilimo," amesema.

Kwa mujibu wa Kawaida, maeneo hayo ndiyo yatakayotumika na vijana wa BBT na wengine watakaokuwa na nia ya kujihusisha na kilimo. Pendekezo hilo la Kawaida linakuja kipindi ambacho Serikali inalenga kuifanya sekta ya kilimo ichangie asilimia 10 katika pato la Taifa ifikapo mwaka 2030.

Akizungumza katika ziara hiyo, Katibu wa CCM mkoani humo, Jonathan Mabihya alipendekeza Wizara ya Kilimo, kupanua skimu za umwagiliaji nchini na kuboresha zile zilizopo.

Alisema katika baadhi ya maeneo wakulima wanatumia majenereta kusukuma maji hali inayowagharimu fedha nyingi takribani Sh500,000 kwa mwezi.

Alitaka Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Nishati kuona haja ya kupeleka umeme.

Aidha, alitaka katika maeneo yenye vyuo vinavyotoa mafunzo ya kilimo kwa vijana, kuna haja ya angalau watu watano hadi 10 kunufaika.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments