Wadau wajadili Rasimu ya Dira ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia.

Wadau mbalimbali nchini wamekutana na kufanya mkutano kwa ajili ya kujadili rasimu ya Dira ya Taifa ya matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

Mkutano huo umefanyika Jijini Dodoma kuanzia Aprili 13 hadi14, 2023 na unawashirikisha wadau mbalimbali kutoka Taasisi zisizokuwa za Serikali na za Serikali.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amewataka wadau mbalimbali walioshiriki mkutano huo kutoa maoni ili kusaidia kuboresha rasimu ya Dira ya Taifa ya kuhamia katika matumizi ya Nishati Safi ya kupikia ifikapo mwaka 2033.

“Nishati Safi ya kupikia ni  nimaelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa lengo ni kumtua mama mzigo wa kuni kichwani ili kuhakikisha kunakuwepo na nishati bora na inayopatikana kwa urahisi," amesema Mramba.

Mhandisi Mramba amesema Serikali kupitia ofisi ya Makamu wa Rais imeelekeza Taasisi za Umma na binafsi zenye watu zaidi ya 300 kusitisha matumizi ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupika chakula ifikapo Januari 31, 2025.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalamu ya Kikundi Kazi ametoa rai kwa wadau wa Sekta binafsi kuchukua katazo lilitolewa na Serikali kama fursa ya uwekezaji. 

 “Katazo hili ni fursa ya uwekezaji katika sekta ya nishati ya kupikia na huu ndio wakati wa kuleta suluhisho la nishati mbadala ya kupikia ambayo itakuwa safi, nafuu na endelevu ili kukidhi mahitaji yaliyopo ikiwa ni sehemu ya jitihada za kitaifa za kufikia asilimia 80 ya matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini ifikapo mwaka 2033,” amesema Mbuttuka.

Wadau kutoka Taasisi mbalimbali nchini wameipongeza Serikali kwa jitihada zinazofanyika ili kuhakikisha inafanikiwa kupata Dira ya Taifa ya kuhamia katika matumizi ya Nishati Safi ya kupikia ifikapo mwaka 2033.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba akizungumza wakati alipokuwa anafungua kikao kilichowakutanisha wadau kwa lengo la kujadili rasimu ya Dira ya Taifa ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia Jijini Dodoma.
                                        

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka akiongoza mjadala  wakati wa kikao kilichowakutanisha wadau mbambali ili kujadili rasimu ya Dira ya Taifa ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia.
                                         

Kamishina wa umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kulia) akifuatilia  mjadala wa rasimu ya Dira ya Taifa ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia.

Wadau mbalimbali walioshiriki kikao cha kujadili rasimu ya Dira ya Taifa ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kilichofanyika April 13, 2023 jijini Dodoma.

Wadau mbalimbali walioshiriki kikao cha kujadili rasimu ya Dira ya Taifa ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kilichofanyika April 13, 2023 jijini Dodoma.


Na Timotheo Mathayo, Dodoma. (Picha zote na Godfrey Mwemezi.)TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments