Wanahabari wapewe mbinu za mabadiliko ya sheria ya Habari

Wakati wadau wa sekta ya habari wakitaka baadhi ya vifungu vya Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 viondolewe kwa kuwa vinaminya uhuru wa habari, wabunge wamewataka waandae hoja madhubuti za kushawishi mabadiliko wanayoyataka.

Ushauri huo wameutoa Aprili 25,2023 mara baada ya kukutana wadau wa Haki ya Kupata Habari (CoRI) wanaoongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, Neville Meena, Deus Kibamba na James Marenga waliokwenda bungeni jijini Dodoma kuwashawishi wabunge wapitishe vifungu vitavyokuza tasnia ya habari.

Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndungulile amesema wabunge watakuwa na fursa ya kujadili muswada wa marekebisho ya sheria hiyo uliopelekwa bungeni Februari 10 mwaka huu, hivyo ni wakati mwafaka kwa wadau kuwaelimisha wabunge juu ya mabadiliko wanayoyataka.


“Muwe na ufafanuzi halisi na unaoweza kushawishi wabunge, tena kwa mifano. Mfano mnataka kusiwepo na leseni, je, nchi nyingine zinafanyaje, hasa za Afrika. Kila hoja mnayoitoa iwe na ufafanuzi mzuri kwa wabunge,” amesema Ndungulile.

Mbunge wa Mafinga, Cosato Chumi amesema sheria zinapaswa kuendana na mabadiliko makubwa ya teknolojia ili ziweze kutekelezwa kwa urahisi na ufanisi.

Chumi ametoa kauli hiyo baada ya Balile kumueleza madhara ya kuwa na sheria za habari zinazoshusha taswira ya Tanzania kimataifa.

Balile amesema kuwa na sheria inayokataza kuingia nchini kwa machapisho ya nje bila kuweka vigezo halisi kunasababisha Taifa kuingia kwenye orodha ya mataifa yanayonyonga uhuru wa habari.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments