Zambia, Malawi kushirikiana na Tanzania sherehe za Muungano

Naibu Waziri wa Nchi  Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Khamis anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 59 ya  Muungano wa Tanganyika na  Zanzibar zitakazofanyika   katika mji wa Tunduma Mkoa wa Songwe mpakani mwa Tanzania na Zambia.

Sherehe hizo ambazo zimeratibiwa na Halmashauri ya Mji wa Tunduma kwa kushirikiana na Kampuni ya Edwin Luvanda Branding Entertainment  zitashirikisha watu zaidi ya 1,300 wakiwepo viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, watumishi wa Serikali  na raia  zaidi 150 kutoka nchi jirani ya Zambia na Malawi.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Aprili 21, 2023  mratibu wa sherehe hizo, Furaha Mapunda amesema  lengo ni kuenzi Muungano sambamba na kijadili  masuala mbalimbali ya fursa za kiuchumi kwa maslai mapana ya Taifa ikiwepo mmonyoko wa maadili.


“Hili ni tukio la kwanza kufanyika katika Mikoa ya Nyanda za juu kusini na sababu ya kufanya katika mji wa  Tunduma ni kujenga mahusiano mazuri baina ya viongozi,wananchi wadau kutoka  mikoa ya Mbeya na Songwe sambamba na raia wa nchi jirani ya Zambia ambao kuna mashirikiano  ya shughuli za kiuchumi kupitia mpaka wa Tunduma,”amesema.

Mapunda amesema katika kuadhimisha sherehe hizo  wanatarajia kuwa na makundi makubwa mawili  la kwanza litafanyika mchana litashirikisha watu  zaidi ya washiriki 1,000 ambao watafanya masuala mbalimbali ikiwemo maonyesho ya makabila na tamaduni, michezo huku kundi la watu 300 watashiriki usiku wa Muungano.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni Luvanda branding Entertaiment, Edwin Luvanda amesema kutokana na ukubwa wa tukio kushirikisha raia kutoka nchi zinazopakana na Tanzania hali ya ulinzi na usalama imeimarishwa.

“Ni tukio la kwanza kukutanisha viongozi  wa Mkoa wa Mbeya, Songwe na raia wa nchi jirani za Malawi na Zambia, ambao watajifunza mambo mbalimbali ikiwepo amani iliyopo ambayo inakutainisha viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, dini na wadau mbalimbali pamoja,”amesema.


Luvanda amesema miongoni mwa viongozi watakaoshiriki ni pamoja  Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala, viongozi wa kisiasa kutoka vyama mbalimbali Mkuu wa Mkoa wa Songwe,  huku Mkoa wa Mbeya wa Mbeya Juma Homera atawakilishwa na Mkuu wa Wilaya Beno Malisa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Daudi Shubata amesema wameamua sherehe za Muungano katika Mkoa wa Songwe ni kuenzi tunu zilizoachwa na hayati Mwalimu Julius Nyerere na Amani Abeid  Karume na kuonyesha mataifa na nchi jirani kuona umoja wa  nchi ya Tanzania katika kujenga ushirikiano ulioachwa na wahasisi.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu Ofisa elimu Mkoa wa Songwe, Michael Lugola amesema tayari wameanza maandalizi na wanatarajia kupokea wageni kutoka nchi za Malawi na Zambia kushiriki sherehe za Muungano Aprili 26 mwaka huu.

“Hii ni fursa pekee za   kiuchumi katika Mkoa wa Songwe kwa wafanyabishara kwani watapokea ugeni mkubwa ambao pia utachoche kuongezeka kwa mapato ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma,”amesema.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments