Hayo yamebainishwa leo Jumatatu Mei 15, 2023 na kiongozi wa Shamba hilo Naweed Mulla wakati wa uzinduzi wa mradi wa kilimo cha mazao ya malisho ya mifugo uliofanywa na kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Abdallah Kaimu.
"Wafanyakazi wote wanaishi hapa hapa na kwenye eneo la mradi na familia zao na nimefanya hivyo kwa lengo la kuwawekea mazingira bora ya kuishi," amesema.
Amesema kuwa kutokana na changamoto za ya uhaba wa malisho ya mifugo ambao umekuwa ukisababisha migogoro ya ardhi baina ya Wakulima na wafugaji, taasisi yake imeamua kujikuta kuzalisha mazao ya mifugo ambapo atakuwa anawahudumia wafugaji.
Kwa upande wake Mbunge wa Chalinze (CCM) Ridhiwani Kikwete amewataka wakazi Wilayani humo kuunga mkono juhudi za Serikali hasa kutunza mazingira na kulinda vyanzo vya maji.
Kikwete amesema kuwa Serikali iko bega kwa bega na wawekezaji hasa wanaoweka miradi inayosaidia jamii kwa nyanja mbalimbali ikiwemo ajira na kulipa kodi ya Serikali.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023, amewataka wakazi wa Wilaya hiyo kutofanya shughuli za kibinadamu jirani na vyanzo vya maji na badala yake kuwa walinzi Ili kuhakikisha vinasaidia vizazi vilivyopo na vijavyo
Mbali na hilo pia kiongozi huyo amewahimiza wakazi hao kujilinda kiafya dhidi ya maambukizi ya magonjwa Ili kuwa na afya njema na kushiriki shughuli za maendeleo.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema kuwa Mwenge wa uhuru utazindua jumla ya miradi 99 yenye thamani ya tilion 4.4.
0 Comments