BARAZA LA MADIWA LUDEWA, LAMMPONGEZA RAIS

 Baraza la madiwani wilayani Ludewa mkoani Njombe limetoa salamu za shukrani na pongezi kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ulipaji fidia kwa wananchi wanapisha mradi wa Liganga na Mchuchuma.


Akiwasilisha taarifa mbele ya baraza hilo mmoja wa wajumbe ambaye ni Diwani wa Kata ya Milo Robert Njavike amesema fedha za fidia hizo zilikuwa zikisubiliwa kwa miaka mingi na wananchi hao kiasi cha kukata tamaa hivyo ujio wa fedha hizo umeinua tumaini jipya.

Hoja hiyo iliungwa mkono na baraza zima la madiwani ambapo Diwani wa kata ya Ibumi Edward Haule sambamba na Diwani wa kata ya Manda Elfrida Kizota wakiainisha miradi mbalimbali iliyofika wilayani Ludewa na kunufaisha wananchi huku Diwani wa kata ya Lupingu ambaye ni diwani kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akikiri kuona maendeleo yanayofanywa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi kupitia Rais Dkt. Samia.

Stanley Kolimba ni mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi wilayani humo lakini pia aliwahi kushika nafasi ya ubunge wa Jimbo la Ludewa Stanley Kolimba amesema wabunge wengi wamepiga kelele juu ya ulipwaji fidia na kuanzishwa kwa miradi hiyo ya Liganga na Mchuchuma lakini kelele zao hazikuleta matokeo chanya hivyo ametoa pongezi kwa Rais huyo sambamba na mbunge wa jimo hilo Joseph Kamonga kwa kufanikisha jambo hilo. 


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments