Chongolo awanyoshea kidole walioanza kujinadi kabla ya muda

 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewanyoshea kidole na kuwaonya wanachama walioanza kujinadi kutaka nafasi mbalimbali za uongozi kabla ya muda wa uchaguzi.

 Chongolo amesema nchi nzima hakuna mtaa, kata wala jimbo lililo wazi.

Akizungumza na wanachama wa Shina namba tatu, Tawi la Wambi, Kata ya Boma, wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa Chongolo amesema muda wa kuanza kutafuta nafasi za uongozi bado haujafika na wanaofanya hivyo wanamchokoza.

Chongolo na viongozi wengine walihudhuria kikao cha kawaida cha shina hilo namba tatu.

"Acheni waliopewa dhamana wafanye kazi, acheni Madiwani, Wabunge na Wenyeviti wa Mitaa wafanye kazi. Subiri wamalize muda wao baada ya hapo jitokeze uchukue fomu," amesema Chongolo na kuongeza;

"Viongozi waliopo wasibugudhiwe na Kuna mafaili yamefunguliwa, acheni kuvizia na msiwe na tabia za fisi maana tabia ya fisi ni kusubiri mkono wa binadamu uanguke. Tuache kuingia kuwavuruga,"

Amesema Bunge linatarajia kuvunjwa Juni, 2025 lakini sasa wabunge hawapaswi kubugudhiwa na badala take waendelee kufanya kazi.

"Wakikuamini watakupatia kazi, jiandaeni lakini subirini," amesisitiza kiongozi huyo.

Awali Mbunge wa Jimbo la Mafinga Cosato Chumi akitaja mahitaji ya jimbo hilo amesema miongoni mwa mahitaji ya mitaani ni taa za barabarani ili kuongeza ulinzi na usalama. ameomba kitolewe kibali kitakacho ruhusu biashara zifanywe  kwa saa 24.

"Tunaomba kwenye baadhi ya Miji kama Mafinga biashara iruhusiwe saa 24, najua ipo sheria inataka biashara mpaka saa 4, isiwe hivyo ili miji yetu ikue,"amesema.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments