MKUU
wa Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga Jokate Mwegelo amelishukuru Shirika
la Lions Club International katika juhudi zake za kuungana na Serikali
katika kuboresha huduma ya afya wilayani humo .
Jokate
ameyasema hayo wakati akikabidhiwa viti sita vya magurudumu
‘(wheelchairs)’, jenereta ya 10KVA pamoja na mashine sita za kidijitali
kwa ajili ya kupimia mapigo ya moyo kwa ajili ya kutumika katika
Hospitali ya Wilaya Korogwe.
"Tunalishukuru
shirika hili kwa niaba ya wananchi wa Korogwe mkoani Tanga kwa kuguswa
katika kuokoa maisha ya mama na watoto na vitu ambavyo wamewachangia
vitaweza kusaidia Serikali kuboresha huduma za afya ambazo Serikali ya
Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan imeendelea
kutoa.
"Kama
mnavyofahamu Serikali yetu imejikita katika kuboresha miundombinu
mbalimbali na kutoa huduma hususani katika sekta ya afya ambapo tumeweza
kujenga na kuboresha hospitali ya Wilaya ,kuongeza zahanati na vituo
vya afya, zahanati nyingine zimeboreshwa na kupandishwa hadhi."
Amefafanua
kuwa wilayani Korogwe hakuna kata ambayo haina Zahanati ,vituo vya
afya na hicho ambacho kimefanywa na Lions Club kinakwenda kuongeza kasi
zaidi kwa yale ambayo tayari Serikali wamefanya kwa ajili ya wananchi
wake.
Ameongeza
shirika la Lions Club kwa kuunga mkono kwa asilimia zote Serikali ya
awamu ya sita na wanaahukuru kwa jinsi ambavyo wamejitoa kwa ajili ya
jamii.
"Nitumie
fursa hii kuwaalika kuja katika mbio zetu za akina mama na najua hii
haijawahi kufanyika nchini kwetu Tanzania kwamba wajawazito wanatembea
na wanafanya mazoezi kwa pamoja na wanaungwa mkono na akina baba na
akina mama.
"
Hivyo sisi kama Mamathon Korogwe tutalifanya Mei 28 mwaka huu kuazia
saa 12 asubuhi na tumelenga akina mama wajawazito kutoka vijiji vyetu
zaidi kwani tunataka kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na uzazi na
kutoa elimu juu ya afya ya mama na mtoto kabla hajapata ujauzito.
"Na
kipindi chote akiwa mjamzito,akiwa ananyoshe na namna ya kunyonyesha
lakini afya ya mtoto baada ya kujifungua ni muhimu sana, amesema Jokate
na kufafanua Korogwe kuna historia ambayo si nzuri sana na inajulikana
ya kutupa watoto wao...hivyo tutatumia siku hiyo kuzungumza.
Kwaupande
wake Mwakilishi wa Lions Club International ambaye pia ndio Katibu Mkuu
wa Shirika hilo Bhavika Sajan amesema ni kawaida ya shirika hilo
kurejesha Kwa jamii, na wamekuwa wakihudumu hapa nchini tangu mwaka
1960.
Amesema
licha ya kua wanatoa huduma katika njia nyingi lakini juhudi zao
zimezikita katika maeneo makuu matano ili kuigusa zaidi jamii na
maeneo hayo matano ni miongoni mwa mambo muhimu na yanayosumbua ulimwengu kwa kiasi kikubwa.
Amesema
dira na malengo yao ni kurudisha kwa jamii inayowazunguka,huduma zao
zimejikita katika maeneo kama vile mazingira, kupambana na njaa,
kisukari, macho pamoja na Saratani kwa Watoto.
"Tunasema
kua kila kwenye uhitaji basi Lions tupo na kadri tunavyokua pamoja
ndivyo tunavyotoa huduma nyingi zaidi.Mchango wetu kwa leo ni Jenereta
ya 10KVA, viti sita vya Magurudumu na mashine sita za kidijitali za
kupima Presha.
"Tunatarajia
kuendelea kushirikiana kwa ajili ya kusaidia jamii lakini tunawashukuru
Arun wa Specialised Engineering (T) Ltd, Ukumbi wa Tarangini, Lions
Club of DSM Incredibles na Lions Club of DSM Tanzanites kwa msaada wao
waliotoa kwa ajili ya hospitali ya Korogwe."
0 Comments