Dk Mwinyi aanza kukagua mali za CCM


 Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi ameeleza dhamira yake ya kuzihuisha mali zinazomilikiwa na chama hicho ili ziweze kukiendeleza chama.

Dk Mwinyi ametoa kauli hiyo leo Mei 7, 2023 katika ziara yake kutembelea na kukagua mali za CCM zilizopo maeneo mbalimbali na kuangalia fursa zilizopo sehemu hizo na kuona jinsi ya kuwekeza kibiashara ili kukiinua chama kiuchumi.

“Ndani ya kipindi kifupi cha uongozi wangu natarajia kukiona chama kinawekeza kwa vitendo miradi mingi ili isaidie kukiimarisha,” amesema

Pamoja na kuendeleza na kuanzisha miradi mipya, Dk Mwinyi amesema ipo haja ya kuimarisha nguvu na kuziboresha ofisi za chama hicho kuendelea kuwa na hadhi ya CCM.

Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati akiorodhesha mali za chama hicho, Katibu wa Kamati Maalum NEC, Idara ya Uchumi na Fedha kutoka afisi Kuu ya cha Chama Kisiwandui, Afadhali Taibu Afadhali ameyataja maeneo ya kimkakati yanayomilikiwa na chama hicho ikiwemo eneo la tawi la CCM Mbweni.

Maeneo mengine ni ukumbi wa CCM Maisara Social Hall, nyumba ya kumbukumbu ya Afro - Shiraz iliyopo eneo la Posta ya Kijangwani pamoja na eneo la kituo cha mafuta Kinazini, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Huu ni mwendelezo wa ziara za Dk Mwinyi ndani ya chama kwa kuzitembelea ofisi za chama hicho kwa ngazi zote ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake na kukagua mali zinazomilikiwa na CCM kwa ngazi zote.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments