DKT. NCHEMBA APOKEA RIPOTI ZA SENSA

 

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiwa na Ripoti za Sensa za Mgawanyo wa Idadi ya Watu kwa maeneo ya kiutawala na Idadi ya Watu kwa umri na jinsia baada ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa, kukabidhi ripoti hiyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba (katikati) ambaye alimkabidhi Mhe. Waziri Dkt. Nchemba, Katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango (Treasury Square), jijini Dodoma.


Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa, akitoa maelezo ya awali ya Ripoti za Sensa za Mgawanyo wa Idadi ya Watu kwa maeneo ya kiutawala na Idadi ya Watu kwa umri na jinsia kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb). Ofisi za Treasury Square, Jijini Dodoma. Katikatika ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akipokea Ripoti za Sensa za Mgawanyo wa Idadi ya Watu kwa maeneo ya kiutawala na Idadi ya Watu kwa umri na jinsia kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba (katikati), baada ya kukabidhiwa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali. Dkt. Albina Chuwa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma.Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akionesha Ripoti za Sensa za Mgawanyo wa Idadi ya Watu kwa maeneo ya kiutawala na Idadi ya Watu kwa umri na jinsia, baada ya kupokea kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba, baada ya kukabidhiwa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali. Dkt. Albina Chuwa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akisoma Ripoti za Sensa za Mgawanyo wa Idadi ya Watu kwa maeneo ya kiutawala na Idadi ya Watu kwa umri na jinsia, baada ya kuipokea kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba, baada ya kukabidhiwa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments