Fisi waua 24 Karatu, mkakati wa kuwavuna waja

Jumla ya watu 24 wakiwemo watoto wameuawa na fisi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kwenye Kata ya Endamarariek Wilaya ya Karatu.

Takwimu hiyo imetolea leo Ijumaa Mei 19, 2023 na Mbunge wa Viti Maalum Cecilia Pareso katika swali la nyongeza ambapo amehoji juhudi zinazotajwa na Serikali katika kuwavuna wanyama hao, kwamba zinakinzana na uhalisia.

Katika swali la msingi Pareso amehoji kuna mpango gani wa kuwavuna fisi wanaovamia makazi ya wananchi, kujeruhi na kuua watu katika Kata ya Endamarariek.


Katika majibu yake, Naibu Waziri wa Maliasili Mary Masanja amesema katika kukabiliana na changamoto ya fisi kuvamia maeneo ya watu hususani kwenye Kata ya Endamarariek, Wizara imekuwa ikifanya msako wa fisi katika maeneo husika.

Naibu Waziri amesema katika kipindi cha tangu mwaka 2019 hadi sasa jumla ya fisi saba wamevunwa lakini mpango au makazi 11 ya fisi yameharibiwa.

Waziri amesema kwa kuwa fisi wanaishi katika makundi, Wizara inaendelea kufanya ‘survey’ ili kuyabaini makundi ya fisi yaliyosalia na kuyavunja ikiwa ni pamoja na kuharibu makazi yao.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments