Katibu wa NEC, Itikadi wa Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe Sophia Edward Mjema akizungumza na Waandishi na Wahariri wa vyombo vya Habari Leo Jijini Dar es salaam.
Waandishi na Wahariri wa vyombo vya Habari Jijini Dar es salaam katika kikao na Katibu Mwenezi chama Cha CCM Taifa Mhe Sophia Mjema
........
Katibu wa NEC, Itikadi wa Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe Sophia Edward Mjema amewaomba waandishi wote wa habari kuanza ukurasa mpya wa utendaji wao kazi na chama hich ili kusaidia kuleta mlengo mzuri kutangaza mema yanayofanywa na serikali na kuibua mambo mbalimbali.
Wito huo ameutoa leo Jijini Dar es salaam awali akifungua kikao na Waandishi na wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Nchini ambapo amesema amekiri kuwa kimya tangu ateuliwe kwani alikuwa anaangalia namna ya kuweza kukutana nao na kuzungumza nao kufahamu ni wapi walipo,walipotoka,wanapokwenda kimashirikiano na chama cha CCM hivyo akawapatia muda wa kuzieleza changamoto zao na maoni yao nini kifanyike ili kusitokee sintofahamu wanapokuwa wanatimiza majukumu yao.
Naye Muandishi wa kituo cha Redio one Christopha Jamesi amesema kuwa Waandishi walio wengi wakipitia changamoto kwa Maafisa Mahusiano wa Umma walio katika sekta mbalimbali ikiwemo Wizara na taasisi kwa kuwawekea vikwazo wanapohitani Habari wengine kuandika habari wanavyotaka wao na kutoruhusu kama kuna maovu yanatendeka yasiibuliwe na hizo ofisi kila Ofisi ya CAG inapotoa ripoti utagundua ubadhilifu wa mali za umma wakati ingeibuliwa kabla ya kutokea .
"Sisi waandishi tumechoka habari za kuandikiwa na Maafisa habari sisi tumesoma tunaweza kama umekaa ofisini unaangalia Habari za magazeti asubuhi na TV habari zinafanana inatushushia heshima hata nchi za jirani wanatuona sisi tasnia yetu inaendeshwa na habari PR hakuna utofauti kati ya mwandishi wa chombo kingine hao katibu tusaidie hali ibadilike " amesema Christopha
Naye Muandishi wa Jambo TV John Marwa amesema wametumia fedha zao kushiriki katika shughuli mbalimbali za serikali ikiwemo kutangaza Mikutano mikubwa ya CCM kuhamishwa wakazi Ngorongoro lakini mitandao ya kijamii pamoja na kufanya yote hayo lakini kunapotokea jambo ovu katika jamii wakipiga simu kuomba majibu kuthibitisha hakuna ushirikiano zaidi ya kuyumbishwayumbishwa na wanapotoa habari Mamlaka ya Mawasiliano TCRA kuwalipisha faini hivyo suala hilo liangaliwe kwa umakini.
"kiukweli kupitia Waandishi wa habari kuna baadhi ya majukwaa kuandika dokezo na kupewa bajeti kwenda kukagua miradi ya serikali wakiwa na waandishi wachache ukichunguza wamepeleka majina kibao ya wanahabari huku walioenda ni wachache Kisha fedha walozopewa kujinufaisha wenyewe hilo liangaliwe kwa makini fedha za serikali zinaliwa na wajanjawanja" amesema John
Pia Muandishi wa Habari ambaye ni Mlemavu wa Macho Ally Thabiti ameshukuru sana Katibu huyo muenezi Sophia Mjema kukutana na Wanahabari kujua wanayoyapitia kwani yeye pamoja na hali yake amejitoa kufanya kazi kwa Uzalendo lakini anakutana na vikwazo kunyanyaswa, kudharauliwa na baadhi ya Taasisi za serikali hivyo kupitia kikao hiko kitakwenda kufanya mabadiliko makubwa.
Aidha pamoja na mambo mengine, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Mhe Sophia Mjema akifunga kikao amewahakikishia wahariri na Waandishi wa habari anakwenda kuyafanyia kazi maoni yao na kutatua changamoto wanazokumbana nazo hivyo wawe na Imani na Chama cha Mapinduzi (CCM) kitaendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na waandishi wa habari Nchini katika kuliletea Taifa Maendeleo.
0 Comments