Mbunge alalamikia tozo kwenye kahawa

Mbunge wa Mbozi (CCM), George Mwanisongole ameitaka Serikali kuruhusu soko huria la ili wakulima waweze kuuza zao hilo kama inavyofanyika kwenye mazao mengine.

Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka 2023/24, Mwanisongole amesema haioni kwanini Serikali inaona vyama vya ushirika kama vile msahafu ambao hauwezi kubadilika.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, hata malaika ashuke kutoka mbinguni kuja kuongoza vyama vya ushirika vya msingi (AMCOs), bado wataibia tu wakulima.


“Kuna ugumu gani kuleta soko huru, kuwaruhusu wanunuzi binafsi kama ilivyo kwenye mchele, mahindi viwepo. Lakini wanunuzi binafsi wawepo,”amesema.

Amesema kuna makato wanayokatwa wakulima yakiwemo ya kugharamikia viburudisho na wakienda kiwandani pia mkulima amekuwa akikatwa.

“Haiingi akilini kuwalazimisha waende kwenye vyama vya ushirika ambavyo vina makato yasiyo na kichwa. Wengi wa viongozi wa vyama vya ushirika ni wezi tuna ushahidi wa kila kona. Kesi ngapi zipo mahakamani. Sijui ni kwanini Serikali inaogopa kuruhusu soko huru la kahawa?”amehoji.

Amesema vyama vya ushirika kila kona vimethibitisha kufeli na kuna makato mengi na wizi.

Amesema Bodi ya Kahawa na Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI) wamekuwa wakitoza Sh200, tozo ambayo inatumiwa katika uendeshaji wa vyombo hivyo na kuhoji kwanini Serikali isitenge bajeti.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments