Rais Samia afanya uteuzi, yumo aliyewahi kuwa DC Hai

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa mabalozi nane wakiwamo maofisa wawili kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Pia, yumo Gelasius Byakanwa aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro na mkuu wa mkoa wa Mtwara. Kabla ya uteuzi huo Byakanwa aliwahi kuwa ofisa mkuu wa ubalozi Tanzania Korea Kusini.

Taarifa iliyotolewa leo Mei 22, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imesema uteuzi huo ulianza Mei 10, 2023. Walioteuliwa ni pamoja na Meja Jenerali Ramson Mwaisaka, kabla ya uteuzi huo alikuwa mkuu kamandi ya Jeshi la Wanamaji.

Post a Comment

0 Comments