Rais Samia kuongoza waombolezaji kumuaga Membe

Rais Samia Suluhu Hassan, leo Mei 14, 2023 anatarajiwa kuwaongeza mamia ya waombelezaji waliofika katika viwanja kwa Karimjee kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Bernard Membe.

Membe alifariki asubuhi ya Mei 12, 2023 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam.

Ratiba ya kumuaga Membe ilianza asubuhi ya leo nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam ambako ilifanyika ibada takatifu kabla ya shughuli ya kitaifa kufanyika katika viwanja vya Karimjee.


Viongozi mbalimbali wa Serikali wamewasili katika hafla hiyo akiwemo Naibu Spika Mussa Zungu, Waziri wa Mambo ya Nje, Stargomena Tax na Kamishna wa Uhamiaji, Anna Makakala.

Wapo pia mawaziri na wabunge wa zamani waliowahi kufanya kazi na Membe akiwemo Lazaro Nyalandu, Fenela Mukangara, Stephen Wasira, William Ngeleja na Godbless Lema ambaye ni kiongozi wa Chadema.

Baada ya shughuli ya kutoa heshima za mwisho kukamilika jijini hapa mwili wa Membe utasafirishwa kesho Mei 15, 2023 kuelekea katika kijiji cha Chiponda kata ya Rondo mkoani Lindi ambako maziko yatafanyika Mei 16 mwaka huu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments