Sakata la kikotoo laibuka tena bungeni

Sakata la kikooto limetua kwa nyingine bungeni baada ya Mbunge wa Iringa Mjini (CCM), Jesca Msamtavangu kusema tatizo sio elimu bali malalamiko yako katika asilimia ya kikotoo inayotolewa kwa mafao ya mkupuo.

Tangu Julai mwaka jana Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wamekuwa wakilipa mafao ya mkupuo kwa wastaafu  wakitumia kiwango kitokanancho fomula ya kikotoo kipya.

Hata hivyo, kumekuwa na malalamiko kwa baadhi ya watumishi wa umma kuhusu kiwango hicho.
Akiuliza swali la nyongeza leo Jumanne Mei 9, 2023, Jesca amesema tatizo sio wafanyakazi hawana elimu bali wanalalamikia kiwango kinachotolewa na mifuko hiyo.

“Ni lini Serikali itafanya ule ujumuishi, wapo waliokuwa NSSF wakaenda PSSSF wakalipwa kidogo lakini wanatakiwa kwenda tena kufuatilia NSSF. Mmejipangaje kuwasaidia ili walipwe kwa pamoja,”amehoji Mbunge huyo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi amesema awali wastaafu waliokuwa wakilipwa kwa kikitoo cha asilimia 25 walikuwa wanapata mafao ya Sh44 milioni na pensheni ya Sh800,000 kila mwezi.

Hata hivyo, amesema mabadiliko katika kanuni hiyo, ambayo yanatoa mafao ya mkupuo kwa asilimia 33, mstaafu aliyekuwa akipata Sh44 milioni sasa anapata Sh58 milioni na pensheni ya zaidi ya Sh700, 000.

“Hawa wapo asilimia 81 wananufaika. Kiwango hiki kilikubaliwa na vyama vya wafanyakazi, na ni katika kutengeneza   uendelevu wa mifuko hii. Faida ni nyingi,”amesema.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments