Rais wa Wadau wa Nyuki Nchini Apr. Philemon Kiemi ambaye ni Mwanzilishi, Mmiliki na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kijiji Cha Nyuki Nchini Tanzania yupo kwenye Ziara ya Kikazi Nchini Africa kusini.
Bw. Kiemi Katika Ziara hiyo, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Gaudence S. Milanzi , Counselor Happiness G, na CPA Melchior N. Rweyemamu kuhusu Kufungua Ofisi na Viwanda vya Kijiji Cha nyuki co.ltd katika Miji ya Pretoria, Johannesburg na Capetown.
Aidha Bw. Kiemi Ameeleza kuwa hatua ya Kampuni ya Kijiji Cha Nyuki itawasaidia Wafugaji wadogo Nchini Tanzania, kuunganishwa na Masoko ya Uhakika ikiwepo Africa Kusini hasa wale ambao Kwa Sasa wako viwanja vya Bombardia Mkoani Singida wakiendelea kutafuta Masoko ya Bidhaa zao la Nyuki Kwa kushirikiana na Wadau wengine wa miradi ya Maendeleo Nchini.
0 Comments