UKATILI, UNYANYASAJI WA KIJINSIA MAENEO YA KAZI BADO TISHIO

Mwenyekiti wa kamati ya wanawake Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Rehema Ludanga amesema swala la ukatili wa kijinsia na unyanyasaji mahala pakazi umezidi kushamiri,na kwamba katika maeneo mengi wafanyakazi hasa wanawake hawapewi fursa ya kuonesha uwezo wao


Akizungumza na waandishi wa habari mkoni Morogoro Rehema amesema katika kuadhimisha ya siku ya wafanyakazi Duniani ni vyema serikali ikaandalia kwa kwa umakini maswala ya ukatili wa kijinsia, kwani changamoto hiyo ni kubwa na huwakuta hadi viongozi walio kwenye ngazi mbalimbali.

“ Nitumie fursa hii tunavyo adhimisha siku ya wafanyakazi Duniani kuwaomba viongozi hasa wanaume waache unyanyasaji wa kijinsia, kama kuna kiongozi mwanamke apewe fursa kulingana nafasi yake, kama kunamfanya kazi mwanamke apewe nafasi yake bila ya kujali jinsi” alisema Ludanga.

"Viongozi mara nyingi wanaona aibu kusema kama wananyanyaswa ama kufanyiwa ukatili kwa sababu ya kuangalia mtazamo wake katika jamii unamuonaje, wale watu wa chini wanamuheshimu hawajui kile anachokifanyiwa kwahiyo anaona aibu kutangaza hivyo kuendelea kuumia ndani kwa ndani bila kusema na kitendo cha kukaa kimya kinaruhusu ule ukatili na unyanyasaji unaendele kukua kila siku hadi siku." Alisema

Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo wa TUCTA amesema hapa nchini kila mwaka vijana wanao hitimu elimu ya juu ni wengi zaidi ya wanaobahatika kupata ajira rasmi, suala ambalo huenda ni moja ya sababu ya ongezeko la vijana wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

“Ukosefu wa ajira linaweza pia likawa ni chanzo ambacho kinapelekea vijana wetu kurubunika na kudanganyika kuingia kwenye masuala hayo ya ndoa za jisia moja. Alisema

Aidha ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozw na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza asilimia kubwa ya maombi ya wafanyakazi yaliyo wasilishwa kwenye maadhimisho ya mwaka uliopita 2022 ikiwemo kuboresha maslahi ya wafanyakazi, kulipa malimbikizo ya madeni na stahiki kwa wafanyakazi pia kutoa vibali vya ajira mpya.

Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Dunia ( Meimosi) kwa mwaka 2023 yamepangwa kufanyika kitaifa mkoani Morogoro ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Munngano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments