Wachimbaji wadogo hupoteza asilimia 40 ya dhahabu

Asilimia 40 ya dhahabu inayozalishwa na wachimbaji wadogo mkoani Geita hupoteza kutokana kukosekana kwa elimu na mtumizi ya teknolojia duni.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Ofisi ya Kampuni ya GF Truck inayouza vifaa kuchimba madini, Katibu wa Chama cha Wachimbaji Wadogo Mkoa wa Geita (Gerema), Golden Hainga amesema uduni wa vifaa, zana na mitambo ya kuchakata dhahabu miongoni mwa wachimbaji wadogo unapunguza faida yao kulinganisha na gharama wanazotumia.

“Wachimbaji wadogo hutumia nguvu nyingi na gharama kubwa kuzalisha lakini tija inayopatikana ni ndogo kutokana matumizi ya zana, vifaa na teknolojia duni. Ni muhimu Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine kuwezesha matumizi ya teknolojia bora na elimu sahihi ya kuchimba na kuchenjua madini,’’ amesema Hainga


Amesema elimu sahihi na matumizi ya zana na teknolojia bora itawawezesha wachimbaji wadogo kupata uzalishaji wa zaidi ya asilimia 90 ya dhahabu kulinganisha na kiwango cha sasa cha asilimia 60.

Hainga ameiomba ameziomba kampuni zinazouza zana, vifaa na mitambo ya kuchimba madini kwa kushirikiana na taasisi za fedha nchini kutoa mikopo nafuu kwa wachimbaji wadogo kununua zana za kuchimba madini

Mwenyekiti wa Wanawake Wachimbaji Mkoa wa Geita, Asia Masimba ameunga mkono hoja ya wachimbaji wadogo kuwezeshwa kununua na kutumia vifaa na teknolojia ya kisasa ili kuongeza tija katika shuhuli zao.

“Kwa sasa wachimbaji wadogo wengi hawapati tija ya kutosha kulingana na nguvu na mitaji wanayotumia kwa sababu ya matumizi ya zana na vifaa duni. Matumizi ya zana, vifaa na teknolojia ya kisasa pia utalinda mazingira kwa kupunguza ukataji na matumizi ya miti katika shughuli za kuchimba madini,’’ amesema Asia


Mkurugenzi wa Mauzo na Mawasiliano wa Kampuni ya GF Truck, Salman Karmal amesema tayari kampuni hiyo imeingia makubaliano na taasisi za kifedha kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata mikopo ya kununa mitambo ya kisasa ya uchimbaji na kuchenjua dhahabu kwa gharama nafuu.

“Licha ya wengi wao kuwa na uwezo kifedha, bado wachimbaji wadogo wanakosa sifa za kukopesheka kutokana na kutoweka kumbukumbu ya mapato na matumizi; makubaliano na taasisi za fedha utatatua tatizo hili,’’ amesema Karmal

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments