Wafugaji wamlilia Dk Mpango, ataka mawaziri kukutana

Makamu wa Rais Philip Mpango amemuagiza Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Angelina Mabula pamoja na timu yake, kufika Ngorongoro kutatua mgogoro wa mipaka unaolalamikiwa na wananchi wilayani hapo.

Agizo hilo la Dk Mpango linatokana na ombi la Emmanuel Seludie mkazi wa eneo la sale wilayani hapo kulalamikia tume iliyopewa kazi ya kuweka mipaka katika eneo la Mudito na Kibara kuwadhulumu maeneo yao.

Mwakamu wa Rais ambaye yupo ziarani mkoani Arusha, aliitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kufungua barabara ya mto wa Mbu - Loliondo (km217) mkoani hapo sehemu ya Wasso –Sale km 49.


“Nilikuwa naomba…hayo mashamba ndiyo yanatupatia kipato kwa ajili ya maendeleo yetu, mipaka imekatwa vibaya na kuna watu hawafurahii haya ninayosema naomba nilindwe kuna mipaka imewekwa kikabila,” amefichua mwananchi huyo huku akitaja mipaka pekee isiyo na migogoro kuwa ni Digodigo na Maloni.

Kufuatia malalamiko hayo Dk Mpango amemwelekeza Waziri Mabula kukutana na Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela Mei 22, 2023 kwaajili ya kutatua kero hiyo.

“Kwahiyo wiki ijayo mkuu wa mkoa panga timu yako na Waziri wa ardhi ajipange mmalize mgogoro wa mashamba,” ameagiza.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro Emmanuel Shangai amesema katika jimbo hilo eneo kubwa la malisho limemegwa na kufanywa pori tengefu jambo linalosababisha maumivu kwa wafugaji.

“Serikali inajua umuhimu wa uhifadhi lakini mifugo tuliyonayo pia ni uchumi, wakati wa uwekaji wa ‘beacon’ katika pori tengufu la Loliondo, Waziri Mkuu Kassim Majliwa alielekeza mamlaka husika kukaa na wananchi na ili kupangia matumizi ardhi hiyo, lakini sasa sehemu kubwa ya ardhi imechukuliwa na hivyo kupunguza eneo la malisho,” ameeleza Mbunge huyo.


Kero hiyo ilimpa nafasi Makamu wa Rais Dk Mpango kuielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia eneo la malisho lililopungua na kushughulikia mgogoro uliopo kwa kutafuta mipaka yenye uendelevu wa watu na mifugo yao.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments