Wakazi Morogoro waaswa kutunza mazingira

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023, Abdullah Shaib Kaim amesema kupotea kwa uoto wa asili ni matokeo ya kufanya  shughuli za kibinadamu kwenye hifadhi za misitu na vyanzo vya maji kinyume na miongozo ya kisheria hivyo ni vyema wananchi wakaacha tabia hiyo.

Ameeleza hayo kwa nyakati tofauti katika Wilaya ya Mvomero na Manispaa ya Morogoro ikiwa ni mwendelezo wa mbio za Mwenge wa uhuru mkoani Morogoro ambapo amekemea wananchi kulima kando ya bwawa la Mindu.

Akiwa wilayani Mvomero Mwenge wa uhuru umezindua, kuweka jiwe la msingi na kutembelea miradi nane nyenye thamani ya Sh1.1 Bilioni zikijumuisha fedha kutoka Serikali kuu, Halmashauri, taasisi za Serikali pamoja na wadau wa maendeleo

Amesisitiza kuimarishwa kwa usimamizi Katika utekelezaji wa sheria kulinda maeneo ya hifadhi za vyanzo vya maji huku ikielezwa kwamba athari za mabadiliko ya tabia nchi zimekuwa zikionekana maeneo mengi zaidi nchini.

"Niwatake Wakazi wa Morogoro kuacha kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya Maji kama kukata miti, kulima na ufugaji na vyanzo vya Maji," amesema Kaim

Hayo ameyazungumza kabla ya kuzindua mradi wa utunzaji wa vyanzo vya maji, mazingira na kuzuia uchafunzi na kuendeleza rasilimali za maji, unaotekelezwa chini ya Bonde la Wami Ruvu, katika kijiji cha Tangeni Tarafa ya Mlali,

Afisa rasilimali maji Bodi ya maji Bonde la Wami Ruvu, Martin Kasambala amesema pamoja na uhifadhi mradi huo pia utawezesha kupatikana kwa maji safi na salama katika Bwawa la mindu na mto Ruvu ambavyo ndio vyanzo vya maji vinavyotegemewa na wakazi wa Manispaa ya Morogoro na miko ya Pwani na Dar es Saalam.

Mwenge wa Uhuru ukiwa Manispaa ya Morogoro umetembelea, kukagua, kuweka jiwe la Msingi na kuzindua Miradi 14 yenye thamani ya zaidi ya Sh1 Bilioni


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments