Waziri Mkuu Majaliwa ataka Mahakama ‘iheshimiwe’

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza mamlaka mbalimbali nchini kuheshimuwa hukumu halali zitolewazo na mahakamani na iwapo kuna asiyekubaliana na mamuzi hayo, ni vema kukata rufaa na siyo kushindwa kutekeleza.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Mei 11, 2023 bungeni katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo ambapo Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani (CCM), ametaka kujua kauli ya Serikali kuhusu Mamlaka za Hifadhi kushindwa kurudishia mifugo kwa wafugaji ambao wameshinda kesi.

Mbunge huyo alisema kumekuwa na kilio kikubwa kutoka kwa wafugaji ambao walishinda kesi zao na mahakamani ikaamuru warejeshewe mifugo yao lakini kumekuwa na ukimywa wa muda mrefu kwa mamlaka hizo kutekeleza maagizo hayo halali ya mahakama.


Awali akijibu swali hilo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa, anatambua kuwepo kwa migogoro mingi kati ya wakulima na wafugahji na wafugaji na maeneo ya hifadhi.

“Tunatambua kuwa kuna kesi nyingi ambazo wafugaji walipelekwa mahakamani lakini wengi walishinda kesi zao, hivi karibuni tulisikia wabunge wakilalamikia jambo hilo, nitumie nafasi hii kuomba amri za mahakamani ziwe na utekelezaji,” amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu amesema kwa kuwa ni jambo la kisheria kwamba hakuna anayeweza kupinga amri ya mahakama kwa sababu ni hukumu, basi kama kuna maeneo ambayo yana amri hiyo, basi yatekeleze.

Kauli ya Waziri Mkuu imekuja kukiwa na kelele nyingi kutoka kwa wafugaji ambao mifugo yao ilikamatwa kwenye hifadhi na kupelekwa mahakamani lakini baadhi ya walioshinda kesi hawajarudishiwa mifugo yao.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments