Wachezaji 120 Wachaguliwa Kuunda Timu Ya Mkoa Wa Singida Umiseta Taifa


Jumla ya wachezaji wapatao 120 wamechaguliwa kwa ajili ya kuunda kikosi cha timu ya Mkoa wa Singida kitakachoshiriki katika mashindano ya Umoja wa michezo na sanaa kwa shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya Taifa itakayoanza kutimua vumbi Juni 15 hadi 25 mwaka huu  mkoani Tabora.

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa michezo wa Mkoa wa Singida Bw. Amani Mwaipaja  amesema kwamba wachezaji hao wamechaguliwa kutokana na uwezo na vipaji walivyonavyo  Katika fani ya michezo mbali mbali.

Mwaipaja   Amesema hayo wakati wa halfa ya kutangazwa kwa kikosi cha wachezaji iliyofanyika katika Ukumbi Wa Mwenge Sekondary na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali wakiwemo walimu,Wanafunzi pamoja na wadau wa michezo.

Afisa michezo huyo alisema kwamba wachezaji hao wataingia kambini kwa kipindi cha muda wa siku tano kwa ajili ya kujiandaa na kujinoa vilivyo kabla ya kuanza safari ya kuelekea katika mashindano ya Kitaifa mkoani Tabora tarehe 14 mwezi huu.

"Tunashukuru tulikuwa na wachezaji wapatao 800 hapo awali lakini baada ya kufanya mchujo tumefanikiwa kupata wachezaji wapatao 120 ambao ndio watakaouwakilisha Mkoa wa Singida katika mashindano ya  Taifa mkoani Tabora,"alisema Mwaipaja.

Kadhalika aliongeza kuwa katika mashindano ya mwaka huu wachezaji wamejipanga vilivyo kuweza  kuibuka na ubingwa  wa Kitaifa kutokana na kujiandaa vizuri katika michezo mbali mbali watakayoshiriki.

Katika hatua  nyingine alimshukuru kwa dhati Rais Wa jamuhuli ya muungano wa tanzania Dr. Samia Suluhu Hasani Kwa kuendelea kusapoti michezo ndani na nje ya taifa letu. 




 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments