Recent-Post

CHONGOLO AANZA ZIARA MKOANI DODOMA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI, KUTATUA KERO ZA WANANCHI

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameanza ziara yake mkoani Dodoma kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020-2025 sambamba na kusikiliza changamoto za wananchi kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi.

Chongolo katika ziara hiyo itakayofanyika katika majimbo yote ya mkoa wa Dodoma ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu(NEC) ya Chama Cha Mapinduzi( CCM) Itikadi na Uenezi Sophia Mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri Kuu(NEC) Oganaizesheni Issa Haji Gavu.

Katibu Mkuu Chongolo ameanza ziara hiyo kwenye Wilaya ya Mpwapwa yenye majimbo mawili ya uchaguzi .Majimbo hayo ni  Mpwapwa Mjini pamoja na Kibakwe.

Alipofika jimbo la Mpwapwa Chongolo ameshiriki kikao cha ndani cha CCM, pamoja na kupokea taarifa ya hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika Wilaya ya Mpwapwa na Mkoa wa Dodoma kwa ujumla.Pamoja na mambo mengine ziara ya Chongolo imelenga kuhamasisha uhai wa CCM kuanzia ngazi ya shina.

Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameanza ziara yake mkoani Dodoma kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020-2025 sambamba na kusikiliza changamoto za wananchi kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi.

Chongolo katika ziara hiyo itakayofanyika katika majimbo yote ya mkoa wa Dodoma ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu(NEC) ya Chama Cha Mapinduzi( CCM) Itikadi na Uenezi Sophia Mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri Kuu(NEC) Oganaizesheni Issa Haji Gavu.

Katibu Mkuu Chongolo ameanza ziara hiyo kwenye Wilaya ya Mpwapwa yenye majimbo mawili ya uchaguzi .Majimbo hayo ni  Mpwapwa Mjini pamoja na Kibakwe.

Alipofika jimbo la Mpwapwa Chongolo ameshiriki kikao cha ndani cha CCM, pamoja na kupokea taarifa ya hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika Wilaya ya Mpwapwa na Mkoa wa Dodoma kwa ujumla.Pamoja na mambo mengine ziara ya Chongolo imelenga kuhamasisha uhai wa CCM kuanzia ngazi ya shina.

Post a Comment

0 Comments