JAMII YATAKIWA KUSIIMAMIA MAJUKUMU YAO IPASAVYO KWA WATOTO

Wazazi, walezi na jamii kwa ujumla imetakiwa kusimamia majukumu yaoipasavyo kwa watoto kuanzia mwaka sifuri hadi miaka name lengo ni kuwalinda na athari mbalimbali ikiwemo ukatili pamoja na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

Wito huto umetolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Tanga Dalmia Mikaya
alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika Jijini Tanga.
.
Katika maadhimisho hayo halmashauri ya jiji la Tanga imetoa msaada wa
vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwenye vituo vya kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu ambapo katika kituo cha Nyumba ya furaha imetoa kilo 20 za mchele, kilo 40 za Maharage na vyandarua 10 wakivipatia vituo 6 vilivyopo hii ikiwa ni njia ya kuonyesha kuwajali na kuwathamini watoto hao

Mikaya amesema kutokana na mabadiliko ya kidigital Duniaimebadilika sambamba na matukio mengi ya kiukatili dhidi ya watotoyakishamiri hivyo wazazi, walezi na jamii kwa ujumla wana jukumu kubwa
la kuhakikisha wanakiandaa kizazi ambacho kitakuwa ni tegemeo la kesho.

"Wazazi walezi tunapaswa kujua kwamba mtoto naye ana haki yake, ikiwemo kusikilizwa, kulindwa na kuangaliwa kwa umakini niwaombe sana wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuzingatia usalama wa mtoto kuanzia mwaka 0-8 ili tuwe na Taifa lenye vijana waadilifu baadaye ambao watalisongeza taifa letu mbele katika mbalimbali za kiuchumi" Alieleza Katibu Tawala huyo

Amesema kuwa kuna mambo mengi ambayo sasa hivi yanaendelea katika jamii. Alieleza kuwa dunia imebadilika na ipo kwenye mfumo wa 
kidigital ambapo kuna mambo mengi yanafanyika wakati huu ikiwemo ukatili kwa watoto ,unyanyasaji , ubakaji, matumizi mabaya ya mitandao kuna Uhuru mkubwa sana upo kwa watoto, amesema Mikaya.

Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii wa jiji la Tanga Simon Mdende  amesema bado hali ya unyanyasaji kwa watoto hususan kuanzia miaka sifuri hadi miaka nane katika jamii si shwari licha ya elimu inayoendelea kutolea katika jamii kwa maslahi ya mtoto huku. Mdende aliwataka wahisani mbalimbali kujitokeza kuvisaidia vituo vinavyolea watoto ili waweze kupata malezi na huduma bora wanazostahili.

Alieleza kuwa katika halmashauri ya jiji la Tanga kwa watoto wanaoishi kwenye halmashauri ya jiji la Tanga hali si nzuri sana kwa sababu watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wamechukuliwa kutoka sehemu tofauti na wengi wanapowatoa kwenye mazingira waliyozoea wanaathirika
kisaikolojia. “Katika hivi vituo wanapoishi hawa watoto bado uchumi sio mzuri sana kwa hiyo jamii inahitajika sana kujitoa na kusaidia hawa watoto ili kupata huduma mbalimbali" alisema Mdende.

Kwa upande wake Afisa ustawi wa jiji la Tanga Deogratias Casmiri amewataka wazazi na walezi pamoja na majukumu mengine kukaa karibu na watoto kubaini changamoto zinazowakabili katika mazingira ya nyumbani na mashuleni na hatimaye kuzitatua mapema kabla hawajaathirika kwa
namna yeyote ile ili kuwa na kizazi bora Cha baadaye.

"Tusipoweka nguvu ya kutosha katika malezi ya watoto ustawi wa watoto hatuupati, ustawi wa mtoto maana yake apate huduma zote za msingi ikiwemo chakula, malazi, elimu muda wa kukaa karibu na
wazazi, walezi wake , Usimamizi wa haki za mtoto unaanzia kwa mazazi mlezi na jamii yote kwa ujumla kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu jukumu la kuwaangalia watoto ni la kila raia" alisema Casmiri.

Wakizungumza mara baada ya kupokea misaada hiyo mkurugenzi wa kituo cha Goodwill and foundation Sayid Muhzari Aidarus na mlezi wa kituo cha Nyumba ya Furaha Sister Sarah Francis wameeleza hisia zao juu ya msaada hi uliotolewa na halmashauri wakiwataka wadau na wahisani
mbalimbali kuendelea kujitokeza kusaidia watoto waliopo katika vituo hivyo hii Ni kutokana na mahitaji yao huku vituo vikielemewa kutokana na uchumi mdogo.

"Kwa niaba ya taasisi niwapongeze na niwashukuru sana kwaajili ya tukio hili adhimu na lenye thamani juu ya mtoto, watoto Hawa Wana ufahamu na pale wanapoona jamii haiitikii kuja kwao wanahisi kwamba wametengwa kwahiyo tusipokuja Kama hivi Tutajenga Taifa la watu wenye
roho mbaya na roho ngumu kwa sababu wataona hawapotezi chochote kwahiyo kuja kqenu mmewakilisha mamilioni ya watanzania" alisema
Aidarus.

"Kwa niaba ya masister na watoto wa kituo cha Nyumba ya Furaha tunashukuru sana kwa yale yote ambayo mmetutendea Kama serikali katika kituo chetu na vituo vyote ambavyo mnatoa misaada hii Hawa watoto tuliokuwepo nao Wana mahitaji ya vitu vingi na hqki zao za msingi zinatakiwa zitolewe Kama watoto wengine waliolelewa na wazazi
wawili" alisema Sister Sarah.

Siku ya mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa kila mwaka kwa mwaka huu kauli mbiu ni "Zingatia usalama wa mtoto katika ulimwengu wa kidigital.TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments