Kamati yataka sheria, adhabu hoja za CAG

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema ni muhimu kuweka adhabu kwa maofi sa masuuli wanaoshindwa kutekeleza mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Mwenyekiti wa PAC, Naghenjwa Kaboyoka amesema hayo bungeni Dodoma jana jioni wakati anasoma taarifa kuhusu utekelezaji wa maazimio ya bunge yatokanayo za taarifa za CAG kwa mwaka 2020/21. Kaboyoka alisema ni muda mwafaka wa kuboresha sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma hasa katika eneo la adhabu.

Alisema pia kamati imetoa maoni kuwa ni muda mwafaka wa Bunge kuangalia uwezekano wa kuboresha sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia maofisa masuuli kujibu na kutekeleza hoja za CAG na maazimio ya Bunge.

Kaboyoka alisema utekelezaji wa maazimio ya Bunge yatokanayo na taarifa za CAG kwa ukaguzi wa Hesabu za serikali kuu na mashirika ya umma kwa mwaka 2020/2021 bado ina changamoto za kiutekelezaji.

Alisema kamati ina maoni kuwa utekelezaji wa mapendekezo ya CAG kwa miaka iliyopita bado haujafanyika ipasavyo hasa kutokana na uwepo wa mapendekezo 1,104 ambayo hayajatekelezwa kabisa katika serikali kuu na mapendekezo tisa ambayo hayajatekelezwa katika mashirika ya umma.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments