KAMPENI YA HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA YA 'MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN' YAZINDULIWA SHINYANGA

 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (wa pili kulia) akizindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.
Viongozi wakipiga makofi wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign”

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amezindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” inayotokana na azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kwamba msaada wa kisheria unatolewa kwa wananchi wote ili kupata haki, usawa, amani na maendeleo.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo leo Jumapili Juni 11,2023 katika uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga, Mndeme ameiahidi Wizara ya Katiba na Sheria na wadau inaoshirikiana nao katika kuendesha kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria - Mama Samia Legal Aid Campaign kutoa ushirikiano wa hali na mali katika kufikia malengo ya kampeni hiyo ya kutoa msaada wa kisheria kwa watanzania wote hasa wale waishio maeneo ya pembezoni.


Amesema lengo kuu la kampeni hiyo ni kulinda na kukuza upatikanaji wa haki kwa wote kupitia huduma ya msaada wa kisheria nchini hivyo akaagiza kata zote zihakikishe zinatenga maeneo maalum ambayo watoa huduma wataweza kuongea na mwananchi mmoja mmoja kwa faragha.


“Kampeni hii ni utekelezaji wa Katiba yetu. Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 imetambua umuhimu wa upatikanaji haki kwa wananchi kwa kuwa Ibara ya 231(k) ya Ilani imetuelekeza “kuimarisha huduma za msaada wa kisheria hususan kwa wanawake na Watoto katika maeneo yote”, amesema Mhe. Mndeme.


Amesema Kampeni hiyo imekuja katika muda muafaka kwani wananchi wa Shinyanga wana uhitaji mkubwa wa msaada wa kisheria katika nyanja tofauti hususan kuelewa haki zao, wajibu wao, namna ya kutatua migogoro ya ardhi, ndoa, masuala ya mirathi, wosia na utawala bora.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.

“Tumejipanga kikamilifu katika kuhakakisha kuwa wananchi wa Tanzania wananufaika na Mama Samia Legal Aid Campaign. Utekelezaji wa kampeni hii ulifanyika jijini Dodoma tarehe 27 Aprili, 2023, vilevile ilizinduliwa Zanzibar tarehe 9 Mei, 2023. Na awamu hii Kampeni hii imefika Shinyanga, na kupitia huduma hii, msaada wa kisheria unatolewa bure katika Halmashauri zote sita kuanzia tarehe 11 Juni, 2023. Wananchi wote mnaalikwa kushiriki na kupata huduma zinazotolewa”,amesema Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga.


Amefafanua kuwa Kampeni hiyo yenye kauli mbiu ‘Msaada wa Kisheria kwa haki, usawa, amani na maendeleo’ inalenga kuongeza uelewa wa kisheria na haki za binadamu kwa jamii hususan haki za wanawake na watoto, kuimarisha huduma ya ushauri wa kisheria kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia na kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu elimu ya sheria kwa umma, masuala ya haki na wajibu na misingi ya utawala bora.


Madhumuni mengine ni Usimamizi wa mirathi na urithi, sheria ya ardhi na haki ya kumiliki mali na Utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala, hususani kwa viongozi wa Serikali za Mitaa, Watendaji wa Kata, Vijiji, na Wajumbe wa Mabaraza ya ardhi, Wazee wa kimila na Wazee maarufu na Viongozi wa dini.


“Ninatoa wito kwamba sisi sote tushikamane katika kumuunga mkono Kiongozi wetu, Mama yetu, Mlezi wetu na Mtetezi wa Wananchi hususan wanyonge Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania katika kuondoa kadhia na viashiria vyote vya kuminya upatikanaji wa haki hususani ukatili wa kijinsia kwa Wanawake na Watoto ambayo ndiyo changamoto kubwa ya Mkoa wa Shinyanga”,amesema Mndeme.

Ili kuchochea upatikanaji haki na kwa wakati, Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) kushughulikia kesi zote za ndoa, mimba za utotoni na ubakaji ambazo zimekaa muda mrefu katika upepelezi bila kushughulikiwa kwa kuhakikisha watuhumiwa wanapatikana na wanashughulikiwa ili kuondoa changamoto ya kutoroka kwa watuhumiwa pindi wanapopewa dhamana ama wanaposikia wanatafutwa na Jeshi la Polisi.


“Kampeni hii inatukumbusha uwajibikaji na usimamizi wa maamuzi yenye kuleta haki, hivyo niwakumbushe watumishi wote kutojihusishwa na masuala ya rushwa inayopelekea kudhorotesha upatikanaji haki. Katika kutekeleza Kampeni kwa kipindi cha miaka mitatu, tunamuahidi Mheshimiwa Rais tutasimamia maadili kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa haki kwa usawa”,ameongeza Mhe. Mndeme.
Wadau kutoka mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea


“Napenda kutumia fursa hii kuwatambua na kuwashukuru Wadau wa Maendeleo wa Mkoa wa Shinyanga waliounga mkono Serikali katika kufanikisha shughuli ya Uzinduzi wa Kampeni ambao ni Shirika la Umoja wa Mataifa la UNFPA, Barrick Gold mine, NACOPHA, ICS, LSF, WILDAF, TCRS, World Vision, LULEKIA Company,Jambo Group of Companies, Taasisi zote za Umma, Makampuni ya Mitandao ya simu ( HALOTEL, VODACOM na AIRTEL) na Vyombo vyetu vya habari. Tunawashuruku kwa kutambua umuhimu wa shughuli hii kwa watanzania husuan ambao wapo kwenye maeneo ambayo kawaida hawafikiwi na huduma hizi”,ameongeza Mndeme.
 

Akitoa salaamu na kumkaribisha Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amesema Wizara itaendelea kushirikiana na Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar kuhakikisha Kampeni hiyo inatekelezwa ipasavyo ili kuwafikia watanzania kwenye Kata na Mitaa yote nchini.


Mhe. Gekul amesema Wizara ya Katiba na Sheria inamshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kudumisha utawala wa sheria; uzingatiwaji wa haki za binadamu na watu na kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wananchi wote lakini kwa jicho la kipekee kwa wananchi wasiokuwa na uwezo.


“Huduma ya msaada wa kisheria kuwafikia wananchi bure ni mapenzi na upendo mkubwa wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mwananchi wa hali ya chini,” amesema Mhe. Gekul.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul.


“Mhe. Rais Samia anaboresha mfumo wa haki jinai na sasa ameleta msaada wa kisheria bure kwa Watanzania. Naagiza wakurugenzi na wakuu wa wilaya mkasimamie kampeni hii. Niombe kwenu wanashinyanga nendeni mkahamasishe wananchi kwenye maeneo yenu waje wapate msaada wa kisheria. Naomba wananchi hata kama bado haujapata tatizo njoo upate elimu ili uweze kusaidia watu wengine”,amesema Gekul.


“Viongozi wa ngazi zote kuanzia ngazi za vitongoji hadi mkoa muwe na wivu na jambo hili kwani litatatua migogoro mingi katika jamii, elimu itatolewa na wananchi watatatua migogoro yao. Mioyo ya wananchi itapata amani kwani watapata msaada wa kisheria kwani Kampeni hii inagusa masuala ya wosia,ardhi,ndoa, mirathi ambayo yanagusa wananchi wetu", ameongeza Mhe. Gekul.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul.


Akitoa maelezo ya awali kuhusu Mama Samia Legal Aid Campaign, Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo ametaja mafanikio ya kampeni hii toka ilipozinduliwa Mkoani Dodoma na kuendelea katika mkoa wa Manyara kuwa ni pamoja na kusuluhishwa kwa migogoro mingi ya kijamii na hata kifamilia iliyohusu ardhi iliyodumu miaka minne, mitano, na mwingine miaka kumi kulikopelekea watu hawa ambao walikuwa hawasalimiani na hata hawazikani kumaliza tofauti zao.


”Ziko familia ambazo wanafamilia walikuwa hawaongei kutokana na migogoro inayohusiana na ardhi, mirathi na sasa wamesuluhishwa katika Kampeni na wameungana katika kujenga familia zao na taifa kwa ujumla”, amesema Bi. Makondo.


Aidha Bi. Makondo amesema kwa kuwa kuna uwezekano mazingira ya mikoa hiyo kuwa sawa na Shinyanga hivyo uzoefu wa utatuzi wa migogoro hiyo utasaidia Kampeni hiyo kushughulikia masuala yote ya ukatili wa kijinsia, migogoro ya ardhi, mirathi na wosia na kuelimisha jamii kuhusu haki na wajibu wao wa kisheria na kikatiba kwa mbinu na uzoefu uliopatikana mikoa iliyotangulia na hivyo kuwezesha kampeni hiyo kufanyika kwa mafanikio makubwa zaidi katika mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Mwenyekiti wa Uratibu wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria “Mama Samia Legal Aid Campaign”, John Shija.


Naye Kaimu Mwenyekiti wa Uratibu wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria “Mama Samia Legal Aid Campaign”, John Shija ambaye ni Mwenyekiti wa Huduma za msaada wa Kisheria Mkoa wa Shinyanga ameitaja migogoro inayoongoza mkoani Shinyanga kuwa ni ardhi, ndoa, kazi na matunzo ya watoto hivyo kampeni hiyo itakuwa sehemu ya suluhisho la kumaliza migogoro.


"Umuhimu wa kampeni hii ni wa kipekee katika kuongeza wigo wa ufikiwaji haki kwa wananchi, hususani walio vijijini na ambao hawawezi kumudu gharama za mawakili. Kampeni hii imekuwa msingi mzuri wa kujenga uelewa wa wananchi kuhusu haki zao za kikatiba na kisheria. Hii ni kampeni ya miaka mitatu yenye lengo la kufikia mikoa yote nchini huku ikitarajiwa kuhitimishwa mwaka 2026",amesema Shija..


Kwa upande wake, Meneja Rasilimali na Mawasiliano kutoka Legal Services Facility (LSF), Jane Matinde ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kwa maandalizi mazuri kwa ajili ya kufanikisha Kampeni hiyo na kwamba kampeni hiyo itasaidia kusuluhisha migogoro mbalimbali ndani ya jamii na kuongeza uelewa kuhusu haki za binadamu.

Naye Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa amesema CCM ina ofisi katika kata zote hivyo kuahidi kuwa wapo tayari ofisi hizo zitumike kutoa huduma za msaada wa kisheria endapo itahitajika.


Nao wabunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba na Dkt. Christina Mzava wamemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kukubali jina lake litumike katika Kampeni hiyo huku wakisema ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo itasaidia kupunguza migogoro mbalimbali katika jamii.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (wa pili kulia) akizindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga. Wa kwanza Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul. Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa. 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (wa pili kulia) akizindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Mwenyekiti wa Uratibu wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria “Mama Samia Legal Aid Campaign”, John Shija ambaye ni Mwenyekiti wa Huduma za msaada wa Kisheria Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Meneja Rasilimali na Mawasiliano kutoka Legal Services Facility (LSF), Jane Matinde akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Donald Magesa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakicheza wakati Kikundi cha  Shinyanga Arts kikitoa burudani kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Moja ya bango wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakiteta jambo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme  wakicheza na vijana kutoka NACOPHA wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akitembelea mabanda wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Mabanda ya mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria
Wadau kutoka mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Wadau kutoka mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea

Mabanda ya mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria
Mabanda ya mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria
Mabanda ya mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria
Wananchi wakiendelea kupata huduma kwenye Mabanda ya mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria
Wadau kutoka mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea




Picha mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments