James ameyasema hayo Juni 1, 2023 katika Jukwaa la Fikra lililojadili kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi.
Ametolea mfano katika Wilaya yake, jamii ya wahadzabe wananufaika na utunzaji wa mazingira kwa kuuza miti.
"Sio kwamba wana elimu bali ni jambo linalowapa fedha kwa hiyo wenyewe wanapanda miti na kuihifadhi," amesema.
Hata hivyo, amesema vita ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ni endelevu na kila anayekabidhi silaha ahakikishe anafanya hivyo kwa wakati.
Katika mjadala huo, Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima amesema Serikali inapaswa kutengeneza mpango wa kuwatumia watu wanaoishi ngazi ya chini wasambaze elimu.
"Pamoja na hilo, angalau kila mwananchi kwa maana ya kaya ihakikishe inakuwa na miti 10," amesema.
Kadhalika, Padri Kitima ametaka Serikali itengeneze ajira kwa vijana, kwa kuwa pasi na kufanya hivyo watalazimika kuuharibu mazingira kwani ndiyo njia nyepesi ya kupata fedha.
0 Comments