KOCHA NABI AONDOKA YANGA SC

Kocha raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi ameondoka Yanga SC baada ya Klabu hiyo kutangaza rasmi kuachana naye ikiwa ni baada ya yeye kuomba kutoongeza mkataba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Klabu hiyo, imeeleza kuwa Nabi ameomba kuondoka Klabuni hapo ili kutafuta changamoto sehemu nyingine baada ya mafanikio kadhaa yaliyopatikana Klabuni hapo.

Tangu kutua Yanga SC, Kocha Nabi amepata mafanikio ikiwa sanjari na kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu Soka ya  Tanzania Bara (NBC PL), mataji mawili ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), mataji mawili ya Ngao ya Jamii na kuifikisha timu hiyo hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF (CAF CC).

Vile vile, Yanga SC imemshukuru Kocha Nabi kwa mchango wake tangu alipotua Kikosini hapo, huku wakimtakia kila la kheri katika safari yake ya kufundisha soka sehemu nyingine.

Hata hivyo, Uongozi wa Yanga SC umeanza mchakato wa kutafuta Kocha mwengine kuziba nafasi ya Kocha Nabi kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa mashindano wa 2023-2024.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments