Muhongo ashauri bei ya umeme ipunguzwe

Mbunge wa Musoma Mjini (CCM), Profesa Sospiter Muhongo ameshauri kupunguzwa bei ya umeme ili Watanzania wengi waweze kuutumia.

Profesa Muhongo ameyasema hayo leo Jumatatu Juni 19, 2023 wakati akichangia mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2023/24.

Profesa Muhongo amependekeza bei ya umeme ipunguzwe sasa hivi umeme majumbani ni Dola za Marekani senti 9.7 na viwandani ni senti 10.


“Nchi ya Kenya wako juu (bei ya umeme) lakini siyo sababu, sisi tusipunguze bei ya umeme kwa sababu nchi za Afrika Mashariki ni bei ya juu. Bei ikiwa chini watumiaji watakuwa wengi,”amesema.

Hata hivyo, amesema ili uchumi uweze kukua kwa kasi unahitaji umeme wa uhakika na hivyo inatakiwa kufikisha zaidi ya Megawati 10,000.

Aidha ametaja kitu kingine kitakachofanya uchumi kukuwa kwa kasi na kupunguza umasikini ni kuwekeza kwenye uchumi wa gesi mbali na maeneo mengine.

Ameshauri bajeti ijayo kuweka mkazo katika umeme wa gesi trilioni 57.5 ni nyingi lakini hatujafanya kazi zaidi.

“Tanzania lazima tutafute mafuta na gesi kwa bidii zaidi na ndio maana hadi leo ninaamini TPDC (Shirika la Maendeleo la Mafuta) kufanya kazi ya uagizaji wa mafuta na kila mtu hawezi kutafuta mafuta na gesi,”amesema.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments