Naibu Waziri ataka ‘media’ kuwa chachu ya maendeleo nchini

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi amevitaka vyombo vya habari mkoani Mbeya kushirikiana na Serikali katika kuhabarisha umma shughuli za miradi ya Maendeleo zinazofanywa na uongozi wa awamu ya sita.

Mhandisi Mahundi amesema leo Jumamosi June 10, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa salamu kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi aa Habari Mkoa wa Mbeya (MBPC).

Amesema viongozi wa Serikali wanatambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari na itaendelea kutoa ushirikiano wa hali na mali na kutatua changamoto zinazowakabili pindi zinapowafikia


“Tunatambua mchango wenu binafsi tangu nikiwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya, tumefanya kazi pamoja hivyo niwatake kuendelea kushirikiana na Serikali kuona mnakuwa chachu ya kuhabarisha umma masuala mbalimbali yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita,” amesema.

Aidha mhandisi Mahundi ametaka waandishi wa habari mkoani hapa kuendelea kuwa na ushirikiano kupitia umoja huo ambao utaleta chachu na mabadiliko katika nyanja mbalimbali kwa mustakabali mpana wa taifa na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho Nerbart Msokwa amesema viongozi wa Serikali wamekuwa na ushirikiano mkubwa na vyombo vya habari na kwamba wataendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na kuibua changamoto zinazoizunguka jamii

“Tunatambua mchango mkubwa wa viongozi wa Serikali akiwepo Naibu Waziri Mahundi na Mbunge wa Mbeya mjini na Spika Tulia Ackson hivyo kama wanahabari  watatekeleza wajibu wao kutoa taarifa zenye tija kwa maslahi mapana kwa taifa na jamii kwa ujumla,” amesema.

Mwanahabari Samwel Ndoni amesema ni wakati vyombo vya habari kutoa taarifa zenye malengo ya kuelekeza mafanikio taliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments