Rais Samia aomboleza kifo Shirima wa Precision


Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 10, ametuma salamu za pole kwa familia ya Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya shirika la Ndege la Precision Air, Michael Ngaleku Shirima aliyefariki usiku wa Juni 9, mwaka huu katika hospitali ya Aga Khan.

Taarifa za kifo hicho, zilitolewa leo Juni 10 na uongozi wa shirika hilo la Ndege zikieleza kuwa Mzee Ngaleku alifariki usiku wa saa tatu Juni 9 katika hospitali ya Aghakan alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kulazwa Juni 8, mwaka huu.

Rais Samia kupitia mitandao yake ya kijamii ameandika: “Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Michael Ngaleku Shirima, Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Precision Air."

Rais Samia amesema, baada ya utumishi wake wa umma, kwa zaidi ya miaka 30 amekuwa sehemu muhimu katika biashara ya anga na shughuli za kijamii katika nchi yetu.

"Natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, Mwenyezi Mungu amweke mahali pema,"

Taarifa Zaidi za maisha ya Shirima zinaonesha kuwa amekuwa ni mpambanaji wa kihistoria na hata alipoacha kazi shirika la ndege la Air Tanzania alifanya biashara ya kuchoma nyama, baadaye aliendesha malori kwenda Mwanza na alipambana mpaka alipoanzisha shirika hilo la ndege.

Kwa upande mwingine, maisha ya marehemu Shirima yanatajwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwani alikuwa ni mtu wa kujitolea katika jamii na kwamba katika Wilaya ya Rombo ambako ndiko alipozaliwa amefanya mambo makubwa ikiwemo kuanzisha kituo cha watoto yatima na hivi karibu alikuwa anajenga Zahanati kwa ajili ya watoto yatima.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments