Recent-Post

Serikali kuingiza vijana kwenye ufugaji-biashara

Waziri wa Mifungo na Uvuvi ameagiza Bodi ya Maziwa nchini (TDB) kushughulikia programu maalum ya uzalishaji maziwa kwa vijana ya BBT Mifugo ili kuwakwamua kiuchumi na kongezea thamani zao hilo.

Ulega amesema baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuasisi mpango wa vijana wa BBT kwa upande wa Wizara ya Kilimo sasa imehamia Wizara ya Mifugo ambapo kutakuwa na BBT mifugo uzalishaji wa nyama na BBT mifugo uzalishaji maziwa.

Akizungumza leo kwenye maadhimisho ya Siku ya Maziwa Duniani yaliyofanyika mkoani Tabora ametaka bodi ya maziwa kwenda mkoani Mbeya na Kagera mikoa ambayo inazalisha maziwa kwa wingi nchini kuwatafutia vijana maeneo yatakayotumiaka kuzalisha zao hili.


“Nimeiagiza bodi kufanya hivyo kwakua yapo maeneo ya serikali huko vilevile kwa kushirikiana na kampuni za maziwa kama ASAS na Shambani Milk na Benki ya Kilimo na Benki ya biashara kufanikisha jambo hili,” amesema.

“Maziwa ni zao la kimkakati lazima tulirasimishe lazima tutumie sayansi kuliingiza sokoni ili likawe na mchango katika taifa letu hatuna sababu ya kuwa wanyonge katika zao hili” amesema Ulega.

Amesema kwa sasa wanahitaji kuongeza jitihada katika ukusanyaji wa maziwa ili waweze kupanda kutoka asilimia tatu mpaka kufikia kumi ya uzalishaji.

Amesema wanatakiwa kushirikisha wadau ili kujua ni namna gani wanaweza kukaa na kujadiliana njia ambayo itasaidia katika usindikaji wa maziwa wa ndani na kupunguza gharama za kuagiza maziwa kutoka nje.

Aidha kwa upande mwingine amewataka wananchi kupeleka sokoni maziwa halisi na kuacha kuongeza maji, unga, mkojo wa ng'ombe na mitishamba kwani inapoteza ubora na kushusha thamani.

Kwa upande wake Mratibu wa kampuni ya maziwa ya Asas, Mtimila Lipita amesema kampuni yao inaendelea kushirikiana na Serikali kwenye suala zima la ununuzi wa maziwa. Amesema hayo wakati kampuni ya Asas ikiibuka na ushindi wa usindikaji maziwa nchini.


Post a Comment

0 Comments