Katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni meya wa manispaa na mwenyekiti wa chama cha soka la wanawake mkoa wa Singida Bi.Yagi Kiaratu amesema kuwa ni heshima kubwa sana kwa mkoa wa singida kupata mwamuzi bora wa soka la wanawake kwani wapo waamuzi wengi lakini singida tumekuwa bora zaidi.
Bi. Yagi Kiaratu Ametowa witto kwa waamuzi na wanamichezo wengine kuendelea kujitoma na kuwa wavumilivu ilikuendelea kuupa mkoa wetu heshma kwajili ya manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla
Aidha Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa singida (SIREFA) Bw. Hamis Kitila katika hafla hiyo ya kumpongeza Bi.Esta alipata fulsa ya kumpa hongera afisa michezo wa manispaa ya singida Bw. Swamweli Mwaikenda kwa kuendelea kusapoti na kujitolea kukuza na kuendeleza soka la wanawake mkoani singida.
0 Comments