Wasomi watakiwa kuwa nyenzo ya mabadiliko

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema amewataka wahitimu wa elimu ya juu kuwa nyenzo ya mabadiliko chanya katika jamii.

Mjema ameyasema hayo jijini hapa leo, Jumapili ya Juni 11, 2023 wakati akihutubia kwenye mahafali ya seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema kusoma kwao hakujalenga maslahi yao pekee, bali familia zao na jamii inayowazunguka.


"Elimu uliyoipata kaitumie kwa matumizi chanya, tunataka ninyi muwe nyenzo ya mabadiliko," amesema.

Kusoma kwao, alitaka kusiwe sababu ya kuwa wapinzani wa kila jambo, kwa kuwa kufanya hivyo hakuna hatma nzuri.

"Ukiangalia wengi wenu hapa mliohitimu mna zaidi ya miaka 20 ya kuendelea kukua, unaweza kuwa mpinzani lakini angalia maisha yako yanaishiaje," amesema.

Ameisisitiza hoja yake hiyo kwa kufananisha na Taifa la China, akisema kila eneo utakalotembelea katika nchi hiyo wananchi wake wanazungumza maendeleo.

"China kila unapokwenda wanazungumza jambo moja la kujenga nchi, kuleta maendeleo ili wawe wa kwanza," ameeleza.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments