WATANO WAFARIKI NA 20 WAJERUHIWA

Watu watano wamefariki na wengine 20 kujeruhiwa baada ya gari walilokua wakisafiria  Toyota  Coaster yenye namba za usajili T .938 DVQ Lilikua linatokea Mkoani Mbeya Kuelekea Dar es Salaam  kugongana  na Lori la Mzigo lenye namba za usajili  T. 693 DMF katika eneo la Iyovi wilaya ya Kilosa Barabara kuu ya Morogoro - Iringa .

Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Morogoro Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Coaster ambaye jila lake halijafahamika kwa kutaka kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari 

Kwa Upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya St Kizito Mikumi Dokta Steven  Mbilinyi amekili kupokea kwa miili ya watu watano waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

"Tumepokea  miili ya watu 5, wanaume 3  na wanawake 2 na  majeruhi 20 kati yao 10 wametibiwa na tumewaruhusu na 9 wanaendelea kupatiwa matibabu na mmoja amepelekwa hospitali ya Rufaa mkoa Morogoro kwa matibabu zaidi." Alisema Mganga Mfawidhi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments