CCM Kilimanjaro kuwapunguza watendaji wanaokihujumu chama

Chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro kimesema kitawapunguza watendaji wa Serikali ambao watabainika kukitengenezea chama hicho ajali ili kishindwe katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Hayo yamebainishwa leo Jumatatu Julai 24, 2023 na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi wakati akifungua kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho mkoa, ambacho kimeenda sambamba na uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020 – 2025 katika kipindi cha Novemba 2022 hadi Juni 2023.

Boisafi amesema ushindi wao wa mwaka 2024 ndiyo ushindi wa mwaka 2025, hivyo kama wanataka kutengeneza mkwamo ili CCM isifike kule ilikotarajia, hawatakuwa tayari na kwamba watajitahidi kuwapunguza kwa mapema ili chaguzi zijazo ziweza ushindi kwao.


“Tunajua kazi anayoifanya Rais ni kubwa na kama chama ni kuielekeza Serikali yapi yanatakiwa kufanyika, wapi na kwa wakati gani. Tuna ilani yetu ya uchaguzi yam waka 2020 – 2025 na kila mara tunaangalia utekelezaji wake, tunajua ninyi kama watendaji ndiyo mnaoshika mafungu, mkifanya kinyume chake maana yake mnaitengenezea ajali CCM.

“Na sisi kama CCM hatuwezi kukubali kutengenezewa ajali, sisi kazi yetu ni kufuatilia na kuona utekekezaji unafanyika sawasawa. Ninawaomba, tunapojiandaa na mwaka 2024, kama kuna jambo ambalo litakwamishwa na tukabaini ninyi mnakuwa sehemu ya kukwamisha jambo hilo ili tukapate ajali, sisi tutahangaika na ninyi kwa mapema,” amesema.

Ameongeza: “Nawaomba sana watendaji, ushindi wetu wa mwaka 2024 ndiyo ushindi wa mwaka 2025, sasa kama mnataka kutengeneza mkwamo ili sisi tusifike kule, hatutakuwa tayari. Tutajitahidi kuwapunguza kwa mapema ili mwaka 2024 uwe salama na mwaka 2025 ukawe salama.”

Akizungumza wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi, mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdhin Babu amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria kwa watumishi wanaobainika kukwamisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kuendeleza Rushwa, ubadhirifu,uzembe na kushindwa kuwajibika.

“Serikali imeendelea kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria kwa watumishi wanaobainika kukwamisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi kwa kuendeleza rushwa, ubadhirifu na mali ya umma, uzembe na kushindwa kuwajibika kwa namna yoyote ile.

“Niwahakikishie wajumbe wa halmashauri kuu, sisi tulioletwa mkoa wa Kilimanjaro kwa vyovyote vile hatutakuwa sababu ya kukifanya Chama cha Mapinduzi kinakosa kura na kinachukiwa na wananchi,” amesema Babu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments