CCM yaagiza korosho mikoa ya kusini kusafirishwa kupitia bandari ya Mtwara

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeagiza korosho zinazozalishwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara, zisafirishwe kupitia bandari ya Mtwara ili kuzalisha ajira kwa wakazi wa eneo hilo, badala ya kutumia Bandari ya Dar es Salaam.

Kauli hiyo ya CCM inakuja ikiwa ni miaka kadhaa, tangu korosho zinazozalishwa katika Mikoa hiyo zisafirishwe kupitia bandari ya Dar es Salaam.

Mkwamo wa usafirishaji wa zao hilo kupitia bandari ya Mtwara, unatokana na kile kilichowahi kuelezwa na Kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara kuwa, yamekosekana makasha ya kusafirishia zao hilo, tangu ulipozuka ugonjwa wa Uviko-19.


Akizungumza katika mkutano wake na viongozi mbalimbali wa CCM Kanda ya Kusini, Katibu Mkuu wa chama hicho, Daniel Chongolo ameahidi katika msimu wa mwaka 2023/24 korosho zote zitakazozalishwa katika mikoa hiyo, kadhalika zitakazotoka Ruvuma.

“Tumekuwa tukipiga kelele juu ya kutaka korosho zipitie Bandari ya Mtwara tunapiga kelele mwaka na mwaka naimani mwaka huu korosho zote zitapitia hapa hazitaenda Bandari ya Dar es Salaam.

“Tunachokifanya ni maelekezo na maagizo ya ilani ya CCM wapo watu wanahangaika kubadilisha mambo hao ni wazushi wachonganishi na kutengneneza maziria ya kuwagombanisha,”amesema.

Nae Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya uchukuzi) Atupele Mwakibete amesema katika bandari ya Mtwara yameletwa makontena mengi ambayo yatasaidia kutumika kusafirishia korosho kupitia bandari hiyo ambapo awali zilikuwa zikitumia barabara kwenda bandari ya Dar es salaam.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments