Dereva Halima apata mikono ya bandia

Halima Mbwana, ambaye alipata ajali wakati akiendesha basi la kampuni ya Super Feo, iliyosababisha kukatika mkono mmoja, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kufanikisha kupata mikono miwili ya bandia.

Halima ameyasema hayo wakati dua ya shukrani nyumbani kwake wilayani Masasi, aliyoifanya ambapo amemshukuru Rais Samia na Waziri anayeshunghulikia maendeleo ya jamii Dk Dorothy Gwajima, pamoja na wadau wengine.

Kwa mujibu wa dereva huyo, japo alikatwa mkono mmoja, lakini amepokea mikono miwili ya bandia, kutoka WHO, na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).


“Serikali kupitia wizara ya maendeleo, imenipa msaada wa mikono bandia, nilifika kwa Rais Samia Suluhu na kwa Waziri Gwajima kuomba msaada, nashukuru nimepata mikono miwili, mmoja umetolewa na WCF ambao utanisaidia kwa vitu vidogo vidogo ambapo natumia nguvu za mwili, na mwingine nimepewa na WHO ni mkubwa wa umeme,” amesema.

Kwa mujibu wa Halima, mkono huo bandia wa umeme, ni wa kisasa ambao matumizi yake yanahusishwa na moja ya milango ya fahamu ambao ni hisia.

“Nimeandaa dua hii kumuombea Rais Samia, Waziri Gwanjima na Watanzania wote ambao walinisimamia mpaka leo, lakini pia wanafanyakazi wenzangu, hili ni jambo kubwa, sio rahisi. Mtu husukumwa na moyo kufanya kitu, japo niliomba lakini sikuwa nategemea majibu haya, ni ya kushangaza,” amesema.

Naye Nura Abdalla ambaye ni mama mzazi wa Halima, amesema kuwa Serikali na wadau wamemsaidia sana mtoto wake jambo ambalo linampa moyo na kumfanya ajiamini zaidi.

“Serikali imemsaidia mwanangu sana alikutwa na tukio baya lakini Watanzania wengi walimsimamia naye, hali yake kwa sasa inaendelea vinaendelea vizuri. Kupata mikono, hii itampa nafasi ya kusimama tena na kuanza kufanya shughuli mbalimbali za kumuendeleza na kunyanya kipato na familia yake,” amesema.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments